HABARI PICHA : MHE. KATIMBA APONGEZA USHIRIKI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KATIKA MAONESHO YA SABASABA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 1, 2026

HABARI PICHA : MHE. KATIMBA APONGEZA USHIRIKI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KATIKA MAONESHO YA SABASABA


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab A. Katimba (Mb), ametembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, leo Julai 1, 2026.

Katika ziara hiyo, Mhe. Katimba ameipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ushiriki wake katika maonesho hayo, akieleza kuwa hatua ya kuendelea kutoa elimu ya sheria na kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi ni muhimu katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haki na wajibu wao wa kisheria.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki Maonesho ya 50 ya Sabasaba yaliyoanza Juni 28, 2026 na yatakayoendelea hadi Julai 13, 2026. Banda la Ofisi hiyo linapatikana ndani ya Ukumbi wa Karume, ambapo wananchi wanapata fursa ya kupata elimu na huduma mbalimbali za kisheria.



No comments:

Post a Comment