WAZIRI NDUMBARO AWATAKA WASOMI KUWA WAWAZI BILA UPANDE ILI KUELEZA UKWELI KWA JAMII - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, April 25, 2025

WAZIRI NDUMBARO AWATAKA WASOMI KUWA WAWAZI BILA UPANDE ILI KUELEZA UKWELI KWA JAMII




Na Okuly Julius _ DODOMA


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amewataka wasomi nchini kuwa na msimamo usioegemea upande wowote ili waweze kuieleza jamii ukweli pasipo kuwa na upendeleo au ushabiki wa kisiasa.

Dkt. Ndumbaro alitoa kauli hiyo leo, Aprili 25, 2025, jijini Dodoma, wakati wa kufunga maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria ya mwaka 2025 ya Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), yaliyoongozwa na mada isemayo “Nafasi ya Kliniki za Sheria za Vyuo Vikuu katika Kuhakikisha Uchaguzi Huru, Haki na Uwazi Tanzania.”

Akizungumzia suala la uchaguzi, Waziri Ndumbaro alisema kuwa uchaguzi ni haki ya msingi ya binadamu, hivyo kauli ya "No reform, no election" inawanyima wananchi haki yao ya kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia.


Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Elimu, Prof. Razack Lokina, alisema kuwa maadhimisho hayo ni ya nne kufanyika, yakiwa na lengo la kuitangaza Shule ya Sheria ya chuo hicho pamoja na kuhamasisha mijadala ya kisheria kwa jamii.

Naye Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Amina Ally, alisisitiza kuwa licha ya umuhimu wa kuwa na uchaguzi wa haki na uwazi, kulinda amani ya nchi ni jambo la msingi zaidi.

Renatus Mkude, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, alihoji kuhusu majukumu na wajibu wa mawakili na wanasheria katika mchakato wa uchaguzi, akitaka tafakuri ya kina juu ya mchango wao katika kuhakikisha uchaguzi wenye uadilifu.





No comments:

Post a Comment