
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbasi amefafanua kuwa Kanuni zilizotolewa na Benki kuu ya Tanzania kuhusu matumizi ya fedha za kigeni ni kwa ajili ya miamala ya ndani hivyo malipo ya Kimataifa katika sekta ya utalii yataendelea kufanyika kama kawaida.
Amesema Kanuni hizo zimeainisha malipo yanayopaswa kufanywa kwa shilingi lakini pia yale yanayoruhusiwa kufanyika kwa fedha za Kigeni ikiwemo Sekta ya Utalii.
Aidh Dkt. Abbasi amewaahidi wadau wa utalii kwamba hakutakuwa na tozo za ghafla katika kipindi hiki na kwamba ikitokea huko mbeleni wadau wa Sekta ya Utalii watahusishwa kikamilifu.
Dkt. Abbas ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Tatu (3) wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa majadiliano baina ya Sekta ya Umma na binafsi katika utalii uliofanyika Mei 13,2025 jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment