Mbunge wa Jimbo la Mkalama Mhe. Francis Mtinga ameikaribisha Kampuni ya MATI SUPER BRANDS LIMITED kuwekeza katika jimbo la Mkalama kwani wanafanya utaratibu wa kupata maji ya uhakika kama tatizo ni maji
"Tunawakaribisha MATI SUPER BRANDS LIMITED kuja kuwekeza hata kule kwangu Mkalama kwani najua wananchi wangu watapata Ajira na nimuhakikishie kuwa suala la maji halitakuwa kikwazo kwa sababu serikali inatuletea maji kutoka Ziwa Viktoria maana najua ndi kitu pekee kilichowasukuma kuwekeza Babati.
Mhe. Francis ametoa kauli hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara mwaka 2025/2026.
No comments:
Post a Comment