Serikali ya Awamu ya Sita imendelea kutekeleza miradi ya maji ili kuwafikia wananchi.
Moja ya mradi ni mradi wa Miji 28 mkoani Tanga ili kufikia lengo la upatikanaji maji asilimia 85 vijijini na 95 mjini ifikapo mwezi Disemba 2025
Mradi wa maji wa miji 28 wa Handeni - Muheza Korogwe na Pangani ni miongoni mwa miradi inayoenda kubadili na kuleta mapinduzi katika huduma ya maji.
Mradi umelenga kuongeza uwezo wa kuzalisha maji kutoka mita za ujazo 5,500
kwa siku hadi mita za ujazo 52,000 kwa siku. Ni uwekezaji mkubwa uliofanikiwa kwa sapoti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kazi zilizofanyika hadi sasa katika utekelezaji wa mradi imefika asilimia 67.
Ujenzi unahusidha ujenzi wa dakio (water intake) kutoka katika chanzo cha mto Pangani,ujenzi wa chujio, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji, ulazaji wa bomba kuu la maji
urefu wa kilomita 188,na ujenzi wa matenki nane ya kuhifadhia maji yenye ukubwa tofauti.
No comments:
Post a Comment