TUMETOKA AFRIKA KUSINI TUMEKUJA CCM KUJIFUNZA - MAKONYANE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 30, 2025

TUMETOKA AFRIKA KUSINI TUMEKUJA CCM KUJIFUNZA - MAKONYANE



Na Okuly Julius ,DODOMA


Naibu Katibu Mkuu wa Kwanza wa Chama cha African National Congress (ANC), Nomvula Paula Mokonyane, amesema licha ya changamoto mbalimbali ambazo taifa lake limewahi kupitia, bado viongozi mbalimbali wa Tanzania wakiongozwa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, waliendelea kuwaunga mkono na kuwapatia msaada wa hali na mali.

"Hatujaja hapa kama chama cha siasa, bali tumekuja hapa kama watu tuliowahi kushirikiana katika mapinduzi ya Soweto chini ya waasisi wetu, wakiongozwa na Mwalimu Nyerere," amesema.

Ameeleza kuwa ujio wao kwenye mkutano maalum wa CCM haukuwa tu wa kawaida, bali ni fursa ya kujifunza kwa niaba ya Chama cha ANC kuhusu ujasiri, mshikamano na uimara wa Watanzania pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, Mokonyane amekumbusha kuwa wakati nchi yao ilikuwa inapitia kipindi kigumu cha machafuko, Tanzania iliwapokea na kuwafanya kuwa ndugu. Wakati ambapo viongozi wao walikuwa wakitafutwa na kudhulumiwa, Tanzania iliwapokea kwa mikono miwili, na hata leo imeendelea kuwa mfano wa mshikamano wa kweli wa Kiafrika.

"Hii ni historia hai, na sisi hatuwezi kusahau. Leo tunasimama hapa kwa heshima kubwa na tunasema: Asante Tanzania, asante CCM."



No comments:

Post a Comment