
OR-TAMISEMI
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMTA na yale ya Shule za Sekondari UMISSETA kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kuanzia Juni 7,2025.
Mashindano hayo yatajumuisha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, yakihusisha michezo mbalimbali kama soka kwa wavulana na Wasichana,Mpira wa kikapu, Netiboli,Wavu na Riadha.
Michezo mingine ni mpira wa Goli ambao ni maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye uono hafifu, pamoja na Sanaa za Michezo na Burudani ambayo inahusisha ngoma za asili, kwaya na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor).
Mashindano hayo pia yatajumuisha michezo mingine kwa wanafunzi wenye ulemavu, ikiwepo soka Wasichana na Wavulana pamoja na Riadha.
UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 inaratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.



No comments:
Post a Comment