
Deborah Lemmubi-Dodoma.
Mchango wa Vyama vya Ushirika hapa Nchini ni pamoja na kuongeza idadi ya wanachama ambao wamefikia Milioni 10 kutoka wanachama 6,965,272 kwa mwaka 2021/21, Uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushariki, kuongeza Ajira kwa Vijana na Ukusanyaji wa hisa,akiba,Mitaji na uthaminishaji wa mali ya Vyama.
Hayo yamesemwa leo hii Juni 26,2025 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania Bwana Tito Haule wakati akizungumza na Wanahabari kuelekea Maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika Mkoani hapa Julai 5,2025.
Na kuongeza kuwa maadhimisho haya ya siku ya Ushirika 2025 yataadhimishwa tofauti na mingine kwa kuwa umoja Mataifa ulitangaza kuwa mwaka 2025 ni mwaka wa Ushirika wa umoja wa Mataifa tokea ilipoadhimisha kwa mara ya kwanza mwaka 2012.
"Mchango wa vyama vya Ushirika hapa Nchini ni pamoja kuongeza idadi ya wanachama kujiunga katika vyama vya Ushirika ambapo Tanzania tuna vyama vipatavyo 7300 vya Ushirika na wanachama wameongeza kutoka 6,965,272 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia Milioni 10".
Maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yanaongozwa na Kaulimbiu isemayo: "Ushirika Hujenga Ulimwengu Bora kwa Wote". Na yatafuatiwa na maonesho ya bidhaa na huduma ya vyama kwenye kijiji cha Ushirika ambayo yatafanyika viwanja vya 88 Jijini Dodoma.

No comments:
Post a Comment