FDH YAIPONGEZA WCF KWA KUJUMUISHA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA HUDUMA ZAKE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 22, 2025

FDH YAIPONGEZA WCF KWA KUJUMUISHA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA HUDUMA ZAKE



Na Okuly Julius – Dodoma


Taasisi ya Foundation for Disability Hope (FDH) imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua madhubuti za kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuishwa kikamilifu katika huduma za kijamii, ikiwemo kupitia Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa FDH Maiko Salali ameeleza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi katika kushughulikia changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.

Salali ameeleza kuwa WCF ni miongoni mwa taasisi zilizoonyesha mfano wa kuigwa kwa kuwa jumuishi, hususan katika kutoa huduma zinazowagusa watu wenye ulemavu. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Wafanyakazi Sura ya 263, WCF imekuwa nguzo muhimu ya hifadhi ya jamii nchini.

“Tunasherehekea miaka kumi ya mafanikio ya WCF kwa sababu imethibitisha dhamira ya dhati ya kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika mfumo rasmi wa huduma,” amesema Salali

Aidha, Salali amepongeza Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma kwa uongozi wake mahiri na thabiti uliosaidia kuimarisha huduma na kuhakikisha makundi yote yanapata haki sawa.

“Tuna matumaini kuwa katika miaka 10 ijayo, WCF itaendelea kuboresha huduma zake na kuendeleza ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu sawa na makundi mengine ya kijamii,” ameongeza Salali .

Amesisitiza kuwa ushirikiano baina ya taasisi za umma na mashirika yasiyo ya kiserikali ni nguzo muhimu katika kufanikisha ajenda ya usawa na maendeleo jumuishi kwa wote.




No comments:

Post a Comment