HALMASHAURI YA MBULU YASHAURIWA KUANZISHA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI ILI KUPANUA FURSA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 8, 2025

HALMASHAURI YA MBULU YASHAURIWA KUANZISHA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI ILI KUPANUA FURSA

Afisa Ushirika Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania TCDC, Justin Mogendi,akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kwa niaba ya Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara.

Na. Alex Sonna-HAYDOM

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ina Vyama 30 vya ushirika, lakini hakuna chama hata kimoja kinachojihusisha moja kwa moja na sekta ya ufugaji hali inayotajwa kuwa pengo kubwa katika mnyororo wa fursa za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Afisa Ushirika Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania TCDC, Justin Mogendi, wakati akifunga mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kwa niaba ya Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara.

Mogendi amesema kuwa ipo haja ya haraka kwa wananchi kuanzisha vyama vya ushirika vya mifugo ya kuku, mbuzi na ng’ombe ili kufungua milango ya mafunzo, mikopo na masoko ya uhakika.

“Tuna vyama vingi, lakini hakuna vinavyojikita katika mifugo, wakati sekta hii ni uti wa mgongo kwa wakazi wengi wa Mbulu, hili ni eneo ambalo linapaswa kutazamwa upya,” amesema Mogendi.

Mbali na hayo Mogendi ameeleza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni mkombozi kwa wakulima na unapaswa kutumika kikamilifu kupitia vyama vya ushirika vya mazao kama mahindi, alizeti na dengu.

Alibainisha kuwa katika maeneo kama Haydom, uzalishaji wa mahindi ni wa kiwango kikubwa, hivyo kuwepo kwa vyama vinavyoendesha mfumo huo kutasaidia wakulima kupata bei nzuri sokoni na kuepuka hasara za kuuza kwa bei duni wakati wa mavuno.

“Manyara ni miongoni mwa mikoa inayozalisha mahindi kwa wingi, tusipoweka mifumo ya usimamizi kupitia vyama, wakulima wetu wataendelea kunufaisha walanguzi badala ya kujinufaisha wenyewe,” ameongeza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Haydom AMCOS, John Sanka, aliishukuru Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kupeleka wakufunzi, akieleza kuwa mafunzo hayo yamewapa maarifa ya kutafuta soko kabla ya uzalishaji hatua itakayosaidia kupata masoko ya uhakika.

“Ombi letu ni kwa serikali kutusaidia sisi vyama vipya. Mafunzo haya ni chachu, lakini bado tunahitaji msaada zaidi ili kukua,” amesema Sanka

Naye Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Dominick Nzimba, amesema washiriki wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu kanuni bora za kilimo na usimamizi wa fedha, tofauti na hapo awali ambapo uzalishaji haukuwa na mwelekeo wa kiuchumi.

Amesisitiza kuwa wakulima wa mboga mboga nao wanapaswa kujiunga katika vyama vya ushirika ili waweze kufikiwa na mikakati ya kiserikali ya kuwawezesha kwa njia ya urahisi na kwa pamoja.

Afisa Ushirika Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania TCDC, Justin Mogendi,akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kwa niaba ya Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara.

Afisa Ushirika Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania TCDC, Justin Mogendi,akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kwa niaba ya Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara.

Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Dominick Nzimba,akizungumza wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Mwenyekiti wa Haydom AMCOS, John Sanka,akizungumza wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Mtendaji wa Kata ya Haydom Elizabeth Marwa,akizungumza wakati wa mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 yaliyohitimishwa Juni 7,2025 katika Haydom AMCOS iliyopo Haydom Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Sehemu ya wanaushirika wa Haydom AMCOS wakimsikiliza Afisa Ushirika Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania TCDC, Justin Mogendi (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo kwa wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi Kwa awamu ya pili mwaka 2024/2025 kwa niaba ya Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara.

No comments:

Post a Comment