
Na Ferdinand Shayo ,Kilimanjaro .
Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imedhamini mashindano ya West Kili Tour Challenge 2025 msimu wa 5 yanayojumuisha mbio za riadha,baiskeli na piki piki yaliyofanyika katikati ya Hifadhi ya shamba la Miti la West Kilimanjaro kwa lengo la kukuza utalii wa michezo na kuunga mkono juhudi za Rais Dr.Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Kampuni hiyo Brayson Mnene amesema wamekua wakidhamini mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo kwa lengo la kuunga mkono utalii wa michezo na shughuli za uhifadhi zinazofanywa kwa lengo la kutunza ekolojia ya Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Siha Dr.Christopher Timbuka amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya utalii katika hifadhi ya shamba la miti la West Kilimanjaro lenye vivutio mbali mbali vya utalii ikiwemo wanyamapori,ndege na miti ya asili.
Mkuu wa Hifadhi ya West Kilimanjaro Robert Faida ameyataka makampuni mbali mbali kuunga mkono mashindano hayo yanayolenga kutangaza utalii na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta hiyo .
Kwa Upande wake Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godifrey Mzava amewapongeza Waandaaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini kwa kushiriki kwenye tukio hilo kubwa lililowakutanisha mamia ya wananchi na wadau wa utalii








No comments:
Post a Comment