MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI FRED LOWASA AMPONGEZA BILIONEA MULOKOZI KWA KUTOA MSAADA WA VITI MWENDO KWA WATU WENYE ULEMAVU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 21, 2025

MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI FRED LOWASA AMPONGEZA BILIONEA MULOKOZI KWA KUTOA MSAADA WA VITI MWENDO KWA WATU WENYE ULEMAVU



Na Ferdinand Shayo ,Arusha .


Mbunge wa Jimbo la Monduli Fred Lowasa amempongeza Mfanyabiashara maarufu Bilionea David Mulokozi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brands kwa kutoa misaada mbali mbali kwa watu wenye ulemavu ikiwemo viti mwendo kupitia Taasisi yake ya Mati Foundation.

Akizungumza katika kata ya Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha kwenye Halfa ya kukabidhi misaada kwa watu wenye ulemavu ikiwemo viti mwendo ,vifaa vya shule pamoja na gesi zilizotolewa na shirika lisilokua la kiserikali la SYWSO kwa ufadhili wa taasisi ya MATI FOUNDATION iliyoanzishwa na Bilionea Mulokozi kwa lengo la kusaidia jamii .

Lowasa amempongeza David Mulukozi kwa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kutumia sehemu ya faida anayoipata kwenye biashara zake kusaidia jamii ya Watanzania.

Aidha Mbunge huyo amewataka Watanzania kumuenzi kwa vitendo Dr.Reginald Mengi kwa kuwawezesha watu wenye Ulemavu kijamii na kiuchumi huku akimtaka Mfanyabiashara Bilionea David Mulokozi kuendeleza kazi nzuri alizozifanya Mengi kwa kuendelea kutoa misaada mbali mbali kwa makundi maalumu kama ambavyo amekua akifanya mara kwa mara.

Afisa Miradi wa Taasisi ya Mati Foundation Izack Piganio amesema kuwa Taasisi hiyo imekua ikitoa misaada mbali mbali ikiwemo viti mwendo kwa ajili ya walemavu pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahitaji.

Mkurugenzi wa Shirika la SYWSO Omega Mlay amesema kuwa wataendelea kutoa misaada kwa watoto wenye ulemavu katika kata ya Makuyuni kupitia mradi wa “MWENDO WA MATUMAINI” iliyozinduliwa leo .






No comments:

Post a Comment