WAZIRI MAVUNDE AKABIDHI GENERETA LA KISASA KWA SHULE YA SEKONDARI YA BUNGE KUIMARISHA HUDUMA ZA UMEME NA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 1, 2025

WAZIRI MAVUNDE AKABIDHI GENERETA LA KISASA KWA SHULE YA SEKONDARI YA BUNGE KUIMARISHA HUDUMA ZA UMEME NA MAJI


Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amekabidhi genereta la kisasa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bunge lengo ikiwa ni kuendelea kuwasaidia wanafunzi hao kuendelea kupata huduma ya umeme na maji pindi umeme unapokatika.


Mavunde akizungumza baada ya mmakabidhiano amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidiii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Aidha Mavunde amewataka walimu wa shule hiyo kujitoa na kuwasimamia wanafunzi kwa kuwafundisha ili wawasaidie wanafunzi hao waweze kupata ufaulu mkubwa katika shule hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya hiyo ya wasichana ya bunge wamesema genereta hilo litawapa uhakika wa kusoma nyakati za usiku pindi umeme utakapokatika.

Vilevile wamesema umeme unapokatika wanakosa maji lakini kupatikana kwa genereta hilo watakuwa wanapata huduma ya maji kwa muda wote.







No comments:

Post a Comment