Wizara ya Elimu Yazindua Kituo cha Huduma kwa Wateja - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 12, 2025

Wizara ya Elimu Yazindua Kituo cha Huduma kwa Wateja



NA Okuly Julius – Dodoma


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. QS. Omary Kipanga, amesema kuwa uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja katika Wizara hiyo utasaidia jamii kupata elimu kwa urahisi kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika Mtumba, jijini Dodoma tarehe 12 Juni 2025, Mhe. Kipanga alisema kituo hicho ni sehemu ya jitihada za Wizara katika kuongeza uwazi na kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.

"Kupitia kituo hiki, wananchi watapata taarifa sahihi kuhusu sera, mikakati na miongozo mbalimbali ya elimu, jambo litakalosaidia kuongeza uelewa na ushirikiano katika utekelezaji wa mipango ya Serikali," amesema Mhe. Kipanga.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo, alisema uzinduzi wa kituo hicho ni hatua muhimu ya kuimarisha mawasiliano kati ya Wizara na wananchi.

"Kituo hiki kitakuwa kiunganishi muhimu kati ya Wizara na wadau wa elimu. Wananchi sasa wataweza kuuliza maswali, kutoa maoni, pamoja na kupata majibu ya haraka kuhusu huduma zinazotolewa na Wizara," alisema Profesa Nombo.

Kituo hicho kilichogharimu takribani Shilingi milioni 100 kinatarajiwa pia kusaidia katika kuratibu maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji wa sera na utoaji wa huduma bora za elimu nchini.










No comments:

Post a Comment