BALOZI HAMAD NA MWENZAKE WA DRC WAJADILI USHIRIKIANO WA KIHISTORIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 3, 2025

BALOZI HAMAD NA MWENZAKE WA DRC WAJADILI USHIRIKIANO WA KIHISTORIA



Maputo 03 Julai, 2025


Mhe. Balozi Hamad Khamis Hamad amekutana na Mhe. Antoine Kola Masala Ne Beby, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini Msumbiji kwenye Ofisi za Ubalozi huo, Jijini Maputo.

Wakati wa mkutano huo, ambao ni mwendelezo wa mikutano ya Mhe. Balozi Hamad kujitambulisha, Waheshimiwa Mabalozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano wa kihistori kati ya Tanzania na DRC kwa maslahi ya pande zote mbili.

Katika hatua nyingine, Mhe. Balozi Beby ambaye ni Kiongozi wa Mabalozi wa Afrika nchini Msumbiji, alieleza kutambua na kushukuru mchango wa Tanzania kwa nchi yake katika maeneo mbalimbali hususan kwenye ulinzi na usalama.

Naye Mhe. Hamad aliahidi kufanya kazi kwa ukaribu na Mhe. Balozi Beby pamoja Mabalozi wengine wa Afrika waliopo Msumbiji ili kufanikisha Malengo ya Umoja wa Afrika.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Maputo.


No comments:

Post a Comment