
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Dk Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo Julai 12,2025.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango elekezi wa kuimarisha uwezo wa kufanya na kutumia tafiti za kiutendaji katika kuboresha huduma za afya ya msingi. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwa kutambua mchango wake katika uboreshaji wa huduma za afya nchini. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini Dodoma. (Anayekabidhi tuzo hiyo ni Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo kwaajili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwa kutambua uongozi wake mahiri na uwekezaji katika Sekta ya Afya. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri . (Anayekabidhi tuzo hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waganga Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Na Okuly Julius _ DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amesema hali ya utunzaji wa kumbukumbu za dawa na vifaa tiba bado hairidhishi, jambo linalochangia changamoto katika usambazaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD).
Dkt. Mpango alitoa kauli hiyo leo, Julai 12, 2025 jijini Dodoma, wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC).
Mkutano huo wa mwaka 2025 umebeba kauli mbiu isemayo “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote.”
Akihutubia wajumbe wa mkutano huo, Dkt. Mpango alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi na faida za Bima ya Afya kwa wote ili kuwawezesha kupata huduma bora kwa gharama nafuu.
Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Afya kufanya mapitio ya mfumo wa upatikanaji wa dawa za magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) kwenye ngazi ya msingi ya huduma, akisema kuwa dawa muhimu za kisukari, shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo bado hazipatikani kwa urahisi katika hospitali za wilaya na vituo vya afya.
Amesema upatikanaji wa dawa hizo unakwamishwa na miongozo ya sasa ya matibabu (Tanzania Treatment Guidelines), hivyo Wizara inapaswa kuhuisha miongozo hiyo ili kuwezesha huduma bora zaidi kwa wananchi wa kipato cha chini.
Aidha, ameitaka wizara kuimarisha huduma za kliniki zinazotembea (mobile clinics) ili kufikia maeneo ya vijijini na yasiyofikika kwa urahisi.
Dkt. Mpango amesisitiza umuhimu wa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa viapo vya madaktari na wahudumu wa afya, akisema kuwa huduma bora za afya lazima ziende sambamba na maadili ya taaluma, uwajibikaji na uadilifu.
Alizitaka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, pamoja na Chama cha Madaktari kuhakikisha maadili hayo yanalindwa, huku akihimiza hatua kali kwa wote watakaobainika kukiuka viapo vyao, lakini adhabu hizo zitolewe kwa haki bila uonevu.
Aidha, Makamu wa Rais ametoa maagizo kwa Wizara ya Afya kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha suala la ucheleweshwaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya linapatiwa ufumbuzi wa haraka, kwa lengo la kuongeza motisha na utulivu katika sekta hiyo muhimu.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa,,amemshukuru Rais Samia kwa maono yake makubwa na miongozo kwenye sekta ya afya ambayo yameleta mapinduzi makubwa katika kipindi kifupi.
Mhe. Mchengerwa ametumia mkutano huo kutaja mafanikio lukuki yaliyopatikana katika kipindi hiki.
Aidha, amesema mafanikio hayo pia yanatokana na ushirikiano baina ya Wizara yake na Wizara ya Afya.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zilizo na mashine ya kisasa ya uchunguzi na matibabu ya saratani ijulikanayo kama PET Scan, yenye thamani ya shilingi bilioni 18.
Amesema Tanzania ni ya pili au ya tatu Afrika Mashariki kumiliki mashine hiyo, na ya tatu katika ukanda wa SADC. Aidha, Tanzania ni miongoni mwa nchi sita zenye mashine nyingi zaidi za MRI katika ukanda huo.
Waziri Mhagama pia ameeleza kuwa Tanzania imekuwa nchi ya mfano katika matumizi ya teknolojia za kisasa kwenye tiba, ikiwemo upandikizaji wa uloto, huduma za akili bandia (AI) katika upasuaji, tiba za figo, na matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa wagonjwa wa saratani.
Kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2025, Serikali imetenga shilingi bilioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa dawa—ikiwa ni ongezeko kutoka shilingi bilioni 200 zilizokuwa zikitengwa awali. Hii imepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa dawa na vifaa tiba nchini, hasa kwa magonjwa kama UKIMWI, kifua kikuu na malaria.
Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, Dkt. Best Magoma, amesema kuwa kutokana na juhudi za Serikali kuendelea kupanua Sekta ya Afya, mahitaji katika sekta hiyo yameongezeka kwa kasi. Hivyo, wao kama waganga wakuu wa mikoa na halmashauri wanawasilisha mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora unaimarika zaidi.
Dkt. Magoma ametaja mapendekezo hayo mbele ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuwa ni pamoja na kuongezwa kwa ushiriki wa sekta mbalimbali katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko na ili kupata mikakati madhubuti ya kudhibiti maambukizi hayo.
Aidha, wataalamu hao wa afya wamependekeza kila mkoa kuandaa ‘Regional Risk Profile’, ili kutambua viashiria vya athari za kiafya kwa jamii na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo kulingana na mazingira halisi ya mikoa husika.
Pia wamependekeza Serikali kutenga bajeti maalumu kupitia Bohari ya Dawa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya mlipuko, badala ya kutegemea bajeti za vituo vya afya pekee, jambo linaloathiri utendaji wa huduma nyingine.
Mapendekezo mengine ni pamoja na kuwezesha serikali za mitaa kufanya tafiti kuhusu visababishi vya vifo vya uzazi na watoto wachanga, kuongeza ajira mpya kwa kuzingatia mahitaji ya ikama, na kuanzishwa kwa mfumo rasmi wa mafunzo endelevu ya uongozi na usimamizi kwa watumishi wa afya wakiwemo waganga wakuu, maofisa ustawi wa jamii na maofisa wa lishe.
Kwa upande wao, wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali, wakiongozwa na Anthony Mwendamaka kutoka UNICEF, wamesema wamepata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini katika kupanga na kutekeleza afua za afya.
Mwendamaka amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, mageuzi makubwa yameshuhudiwa kwenye sekta ya afya kupitia ajenda ya 4R's — Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding.
Katika mkutano huo wadau mbalimbali wa afya pia wametunukiwa vyeti vya kutambua michango yao.
No comments:
Post a Comment