
Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mradi wa kuboresha elimu ya sekondari-SEQUIP imekamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule mpya za Sekondari za wasichana Dar es salaam na Ruvuma.
Pamoja na dhamira hiyo ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu kwa kuwekeza na kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwenye shule na vyuo, pia ikiwajengea Walimu uwezo wa kiutendaji kupitia mafunzo yanayoendelea kutolewa kupitia mradi wa kuimarisha Shule Salama za Sekondari (SEQUIP).
Katika kutimiza azma ya kuboresha sekta ya elimu nchini, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inatekeleza mradi huo wa SEQUIP kwa thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 500 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 1.2 kwa kipindi cha miaka mitano.
Tangu kuanza kwa mradi huo mwaka wa fedha wa 2021/2022, Serikali imejenga shule mpya za sekondari na kufanya ukarabati mkubwa wa miundombinu pamoja na kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa zaidi ya walimu wa sayansi, wadhibiti ubora wa shule, maafisa elimu wa mikoa, Maafisa ubora wa halmashauri pamoja na walimu wa somo la TEHAMA katika shule za sekondari.
Mkoa wa Dar es salaam na Ruvuma umefanikisha ujenzi wa miundombinu ya shule hizo kwa ufanisi mkubwa hivyo kuwa sehemu ya mikoa mahususi ambayo inatajwa kumkomboa mtoto wa kike, kuimarisha uwezo wake kitaaluma ikiwa ni pamoja na kuzisimamia ndoto zake.
Katika mkoa wa Dar es salam serikali imekamilisha ujenzi wa shule ya Wasichana Dar es salaam kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.450 huku katika mkoa wa Ruvuma ikiwa imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 4.450 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule mpya ya wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan.





No comments:
Post a Comment