NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWAITA WAWEKEZAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 9, 2025

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AWAITA WAWEKEZAJI



Na WMJJWM Dar Es Salaam


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ametoa wito kwa wawekazaji kuwekeza Zanzibar kwa sababu ni sehemu salama yenye mazingira mazuri.

Naibu Waziri Mwanaidi ameyasema hayo mkoani Dar Es Salaam katika siku Maalum ya Zanzibar inayoadhimishwa tarehe 8 Julai 2025 katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (SabaSaba).

Naibu Waziri Mwanaidi amesema kuwa Tanzania ni sehemu salama kwa ajili ya kufanya uwekazaji katika sekta mbalimbali kwani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea kuiongozo nchi katika msingi ya sheria, haki na usawa kwa lengo la kulinda amani na kuweka mazingira rafiki yanayotoa fursa sawa kwa Wawekezaji Wakubwa, wa Kati na Wadogo.

Ameleeza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikihimiza Wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania kujitokeza na kuwekeza katika sekta mbalimbali kwa lengo la kukuza uchumi, kupunguza umasikini, kuongeza fursa za ajira na kuhamasisha matumizi sahihi ya rasilimali kwa lengo la kujiletea maendeleo endelevu.

”Kule Zanzibar upo usemi maarufu usemao “Zanzibar ni Njema, Atakae na Aje”. Nitumie tena fursa hii kuwaribisha watu wote mfike Zanzibar kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji zilizopo zitakazosaidia kuendelea kuimarishaji wa uchumi wa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla” amesema Naibu Waziri Mwanaidi

Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amesema Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imeweka mikakati itakayosaidia kuimarisha mazingira ya biashara, kusaidia urasimishaji wa biashara, kurahisisha usajili wa kampuni pamoja na kuwajengea uwezo wafanyabiashara na wajasiriamali kwa kuwapatia mafunzo mahususi.

Pia Naibu Waziri Mwanaidi amesizitiza Wananchi kutimiza wajibu wao wa kikatiba kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na kuimbea nchi amani na utulivu kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment