PPRA YASHINDA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA MAONESHO YA SABASABA 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 14, 2025

PPRA YASHINDA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA MAONESHO YA SABASABA 2025


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameikabidhi Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Tuzo ya Mshindi wa Kwanza kwa Mamlaka za Udhibiti katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba 2025.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Meneja wa PPRA Kanda ya Pwani, Bi. Vicky Mollel, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Dennis Simba, Julai 13, 2025, wakati wa hafla ya kufunga rasmi maonesho hayo yaliyofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Mollel alisema kuwa PPRA imepokea tuzo hiyo kwa heshima kubwa kwa niaba ya wadau wote wa ununuzi wa umma waliotembelea banda la Mamlaka hiyo na kupata huduma katika kipindi chote cha maonesho.

Aliongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na maandalizi bora na huduma zilizotolewa, ambazo zinaakisi utamaduni wa uwajibikaji na uchapakazi miongoni mwa watumishi wa PPRA, pamoja na uongozi madhubuti kutoka Wizara ya Fedha, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka hiyo.

No comments:

Post a Comment