PROF. MKENDA AZINDUA PROGRAMU YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI AJIRA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 9, 2025

PROF. MKENDA AZINDUA PROGRAMU YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI AJIRA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezindua rasmi Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Ajira inayolenga kufadhili vijana kutoka vyuo viwili vya VETA na chuo kimoja cha Maendeleo ya Wananchi.

Akizungumza Julai 9, 2025 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi Prof. Mkenda alisema kuwa programu hiyo kwa kuanzia itachukua vijana 200 na inalenga kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana wengi ambao wanakuwa na maarifa ya kitaaluma lakini hukosa ujuzi wa vitendo unaohitajika katika soko la ajira pamoja na mitaji ya kuanzisha Biashara

Ameeleza kuwa ili kufanikisha hili ni muhimu kuimarisha uhusiano kati ya taasisi za elimu na viwanda ili kuwezesha vijana kupata ujuzi wa vitendo.

Ameongeza kuwa kuna haja ya kuendeleza kurasimisha maarifa waliyonayo wafanya biashara katika maeneo mbalimbali ya ujuzi na kushirikiana nao katika kufundisha vijana ili wawe na maarifa na ujuzi unaowawezesha kushiriki kwa ajira au kujiajiri.

Prof. Mkenda alisisitiza kuwa programu hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kushirikiana na wadau wa elimu na maendeleo katika kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujifunza, kubuni, na kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa.

Amesisitiza kuwa Serikali imeendelea kuongeza fursa za mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi kwa kuwekeza katika ujenzi wa Vyuo vya VETA katika kila Wilaya nchini na Vyuo vya ngazi ya Mkoa katika mikoa yote nchini lengo ni kihakikishañ kundi kubwa la vijana linapata ujuzi kulingana na shughuli za kiuchumi katika maeneo yao huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia maendeleo ya Teknolojia.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi Ruth Zaipuna amesema kuwa wazo la kuanzishwa kwa programu hiyo lilitoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ambaye alipendekeza benki hiyo itumie taasisi yake kusaidia vijana wa Kitanzania kuweza kujiajiri.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa Vijana watakaonufaika watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali, elimu ya fedha utafutaji masoko pamoja na kupatiwa mitaji kwa njia ya vifaa vya kazi.



No comments:

Post a Comment