Mpango wa Shule Salama umeibuka kuwa chachu ya mabadiliko katika ujifunzaji ndani ya Shule ya Msingi Nasholi iliyopo katika Halmashauri ya Meru mkoani Arusha, kwa kuweka mazingira salama na rafiki kwa wanafunzi yanayowajengea hali ya kujiamini na kujifunza kwa ufanisi.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mpango huo Mwalimu wa Unasihi wa Shule hiyo, Anambora Swai, amesema kuwa umeleta mafanikio katika kuimarisha mahusiano baina ya walimu, wazazi na wanafunzi na kwamba umechangia kuongezeka kwa ushiriki wa wanafunzi darasani na kuboresha mazingira ya kujifunza.
Niwael Mbise, mwanafunzi na Mwenyekiti wa Baraza la Kupinga Ukatili wa Kijinsia shuleni hapo, amesema mpango huo umewajengea uwezo wa kutambua aina za ukatili wa kijinsia na mbinu za kukabiliana nazo, hatua iliyoboreshwa ustawi wao shuleni na hata nyumbani.
Jumla ya shule 3,800 kati ya 6,000 zinazolengwa nchini tayari zimeanza kutekeleza mpango huo, ambapo walimu wanasihi 3,800, walimu wakuu 3,800 pamoja na waratibu elimu kata 680 wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo ili kutekeleza kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment