Na Jeremiah Mbwambo, Bujumbura.
Hayo yamesemwa leo na Mh. Angeline Ndayishimiye mke wa Rais Jamhuri ya Burundi alipokuwa akihitimisha kambi ya Madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyo kuwa ikifanyika nchini Burundi
"Niwape pongezi Madaktari wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mmetusaidia sana kuhakikisha ndugu zetu wanapata matibabu na wanapona, bado uhitaji ni mkubwa sana hivyo tunatarajia mtarejea muda simrefu" amesema Mhe. Angeline
Kwa upande wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi Galasius Byakanwa amesema kuwepo kwa kambi hii ni tafsiri tosha ya kuwafuta machozi, kuongeza furaha na kuokoa maisha ya wagonjwa wa Burundi
"Wagonjwa walioonwa na madaktari wetu ni 2897, katika hawa walio fanyiwa upasuaji ni 211 katika wiki hizi tatu na wote wanaendelea vizuri" amesema Balozi Byakanwa
Ameongeza kuwa wapo watoto ambao wanahitaji kupata matibabu zaidi
"Katika kambi hii kunawatoto 32 wanahitajika kupewa matibabu zaidi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, watoto hawa wanashida ya moyo, hata hivyo ubalozi wa Tanzania nchini Burundi utawasomesha Madaktari wawili walioonesha juhudi ya kujifunza mmoja ni kutoka Hospitali ya Gitega na mwingine ni wa hapa" amesema Balozi Byakanwa
Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kufanya utalii wa matibabu katika nchi za ukanda wa afrika Mashariki na kati, lengo ikiwa ni kutoa huduma hizo kwa wananchi wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment