
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, ameungana na Wakuu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika, kuadhimisha Siku ya Kupambana na Rushwa inayoadhimishwa ALGIERS - Jamhuri ya Demokrasia ya Watu wa ALGERIA.
Wakuu hawa ambao wako Algiers, wanashiriki maadhimisho haya kupitia 'Associstion of African Anti - Corruption Authorities - AAACA', ambao pamoja na mambo mengine watakuwa na Mkutano Mkuu wa 7 wa Mwaka wa Shirikisho hilo, Julai 21 na 22, 2025.
Maadhimisho haya yanafanyika nchini Algeria katika ukumbi wa 'International Conference Center - Abdelatif Rahal, Algiers - Algeria' na kuhudhuriwa na washiriki takriban 250 wakiwemo viongozi kutoka nchi 28 za Afrika.
No comments:
Post a Comment