WANAFUNZI 1,051 KUNUFAIKA NA SAMIA SCHOLARSHIP - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 22, 2025

WANAFUNZI 1,051 KUNUFAIKA NA SAMIA SCHOLARSHIP



Na OKULY JULIUS,OKULY BLOG, DODOMA


Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetangaza kufunguliwa rasmi kwa dirisha la maombi ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2025 kupitia mpango wa Samia Scholarship, huku ikiongeza idadi ya wanufaika kutoka 650 mwaka jana hadi kufikia 1,051 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema kati ya nafasi hizo, 51 zimetengwa mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaokidhi vigezo vya kupata ufadhili huo.

“Wakati tunaanza tulikuwa na uwezo wa kuwafadhili wanafunzi 650 kwa mpigo mmoja. Kwa mwaka huu, bajeti imeturuhusu kufikia wanafunzi 1,051, na kati yao wanafunzi 51 ni wale wenye mahitaji maalum waliopata daraja la kwanza.”.”

Na kuongeza"Dirisha la maombi sasa limefunguliwa rasmi kwa wahitimu wa kidato cha sita 2025 waliopata ufaulu mzuri katika masomo ya Sayansi na wanakidhi vigezo vya kupata ufadhili huu wa masomo ya elimu ya juu," amesema Prof. Mkenda.

Profesa Mkenda amesema wanafunzi 50 watafadhiliwa masomo nje ya nchi katika maeneo ya Akili Unde (Artificial Intelligence), sayansi ya Data na masomo yanayohusiana na fani hizo ambao pia watapaswa kuomba kupitia mpango maalum wa Samia Extended Scholarship.

Amebainisha kuwa wanafunzi watakaomba ufadhili wa Samia Skolashipu Extended watapitia mafunzo ya miezi kumi katika kambi maalum ya maarifa ( Boot Camp) itakayofanyika katika Taasisi ya Nelson Mandela ili kuwaandaa vyema kujiunga na programu hizo pamoja na masuala mengine muhimu ikiwemo uzalendo.

Katika hatua nyingine, Prof. Mkenda ametoa ufafanuzi kuhusu kufutwa kwa baadhi ya kozi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya kitaaluma kwa lengo la kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapo.

Serikali imeendelea kuwekeza katika elimu ya juu kupitia programu ya Samia Scholarship kama sehemu ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Taifa 2050 , ikiwa ni jitihada za kuhakikisha vijana wanapata fursa sawa za elimu yenye tija kwa maendeleo ya nchi.



No comments:

Post a Comment