WIZARA ZATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI NA KUHAMIA MTUMBA KABLA YA OKTOBA – LUKUVI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 23, 2025

WIZARA ZATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI NA KUHAMIA MTUMBA KABLA YA OKTOBA – LUKUVI



Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA 


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri, Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi ameonya Wakandarasi wanosuasua kukamilisha ujenzi wa Majengo ya Wizara na Taasisi katika Mji wa Serikali Mtumba licha ya serikali kutoa fedha.

Ameagiza kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kabla ya Oktoba mwaka huu ili watumishi waweze kuhamia na kutoa huduma kwa wananchi.

Lukuvi ameyasema hayo jijini Dodoma, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo hayo ambayo yanagharimu sh.bilioi 738.

Lukuvi amesema hakuna kisingizio cha kusuasua kwa ujenzin huo kwani Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya kukamilisha.

“Wasukumeni wakandarasi wanaosuasua kukamilisha ujenzi wa kudumu wa ofisi za wizara na taasisi ili watumishi wote wahamie na watoe huduma kwa wananchi.

Ameongeza kuwa :”Tunatamani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu wizara zote ziwe zimehamia Mtumba ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Lukuvi alizipongeza wizara ambazo tayari zimeshahamia licha ya majengo yao kutokukamilika.

Lukuvi amesisitiza ununuzi wa thamani zinazotengenezwa nchi kama ilivyoelekezwa katika mikataba iliyotolewa.

“Tunatamani kuona thamani zote zitakazonunuliwa ziwe za kutoka Tanzania kama tulivyoelekeza katika iataba yenu kwasababu tumebaini kuwa thamani hizo zinadumu kwa muda mrefu,”amesema

Kwa Upande wake Mratibu wa Kikosi cha Kuhamishia Mji wa Serikali Dodoma na Uendelezaji wa Mji wa Serikali Mtumba Noeli Mlindwa alisema ujenzi unahusisha majengo 34 ya wizara na taasisi za serikali.

Amesema hadi hivi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92.2 hadi kukamilika kwake utagharimu sh.bilioni 738.

Vilevile amesema hadi hivi sasa serikali imeshatoa sh.bilioni 544.7 kwa ajili ya sughuli mbalimbali za ujenzi.

“Hadi sasa majengo 10 ya wizara yameshakamilika na watumishi wamehamia na kuanza kutoa huiduma mbalimbali kwa wananchi. Serikali imetenga sh.bilioni 66 kwa ajili ya ununuzi wa Maziku thamani za ofisi ambazo,”amesema

Ameongeza kuwa :”Katika kuhakikisha mji unakuwa wa kijani tunatarajia kupanda miti 253,000 kuzunguka maeneo yote ya mji wa serikali,”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Benjamini Maziku amesema ujenzi wa barabara kilometa 51 katika mji wa serkali Mtumba imekamilika kwa asilima 100.

Amesema pia ujenzi wa barabara hizo ulienda sabambamba na ufungaji wa taa za barabarani na kamera kwa ajili ya usalama.

“Zoezi la ufungaji wa taa za baraarani limekamilika kwa asilimia 100 hivi sasa tunaendelea na majaribio ya taa hizo kwasababu tunamataba wa miaka mitano na mkandarasi na zikileta shida anakuja kubadilisha,”amesema










No comments:

Post a Comment