Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Ahadi ya Serikali ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa katika Wilaya
zote za Mkoa wa Kagera imetekelezwa baada ya Serikali kusaini mikataba
ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220
kutoka Benako, Ngara hadi Kyaka wilayani Misenyi na kituo cha kupoza
umeme cha Benako cha msongo wa kilovoti 220/33, hatua inayotoa uhakika
kwa Mkoa huo sasa kupata umeme wa gridi badala ya kutegemea umeme
kutoka Uganda kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini kwa mikataba hiyo jijini
Dodoma tarehe 25 Agosti, 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kuanza kutekelezwa kwa mradi huo ni
moja ya maelekezo ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa na kiu ya
kutekeleza ahadi ya Serikali kwa wananchi wa Kagera ya kupata umeme
wa uhakika muda wote ili kutekeleza shughuli zao za kiuchumi na
kijamii.

" Kupitia mradi huu, Mkoa wa Kagera kwa mara ya kwanza na wenyewe
unaingia kwenye gridi ya Taifa hasa na hivyo kuongeza uhakika wa
upatikanaji wa umeme hususan katika Wilaya za Bukoba, Muleba, Misenyi,
Karagwe, Kyerwa na maeneo mengine ya jirani, nawahakikishia watu wa
Kagera kuwa Serikali imeshaamua mradi huu ufanyike kwa wakati kwa
miezi 24 tu" Amesema Dkt. Biteko
Dkt. Biteko amesema, Kagera ambayo mahitaji yake ya umeme hayazidi
megawati 47 baada ya muda itakuwa na uhakika mkubwa wa upatikanaji
umeme kwani kutakuwa na njia mbalimbali za kufikisha umeme mkoani
humo ikiwemo Benako- Karagwe hadi Kayaka, Nyakanazi- Biharamulo hadi
Muleba na kuna mradi mwingine mkubwa unaotarajiwa kujengwa kutoka
Ibadakuli hadi Mbarara Uganda wa kV 400. Vilevile kuna mradi wa
uzalishaji umeme wa Kakono wa megawati 87 ambao upo katika hatua za
mwisho za kutafuta Mkandarasi.
Ameongeza kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan pia anaendelea
kutekeleza miradi mingine ya umeme katika maeneo mengine ikiwemo mradi
wa usafirishaji umeme wa kV 400 wa Tanzania- Zambia, mradi wa
Usafirishaji umeme wa kV 400 Chalinze-Dodoma , mradi wa usafirishaji
umeme wa Mkuranga -Pwani ambao utapeleka umeme kwa wananchi wa
Kusini, pia mradi wa usafirishaji umeme wa gridi imara wa Tunduru-
Masasi- Mahumbika ambao pia unaenda kutoa uhakika wa umeme katika
mikoa ya Kusini.
" Utekelezaji wa miradi hii yote ya umeme ni kielelezo kuwa, Rais,
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaonesha njia ya kuwafikishia wananchi
umeme wa uhakika sasa kinachohitajika kwa watendaji ni kukimbia badala
ya kutembea kwani kinachotakiwa ni matokeo na siyo kusema sana."
Amesisitiza Dkt. Biteko
Pia Dkt. Biteko amewashukuru wafadhili wa mradi ambao wametoa Dola za Kimarekani takriban milioni 105.6 ambazo ameagiza kuwa zitumike kwa
usahihi ili kuwapa sababu wafadhili wengine kuendelea kusaidia miradi
mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko ameagiza TANESCO kuhakikisha
wananchi 1,014 wanaopisha mradi wanalipwa fidia yao mapema
iwezekanavyo yaani kuanzia mwezi septemba mwaka huu.
Aidha, amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi
Felchesmi Mramba, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi
Innocent Luoga na watendaji wa TANESCO kwa kuendelea kusimamia kwa
umakini Sekta ya Nishati.
Vilevile, ameipongeza TANESCO kwa kuendelea kuboresha utendaji wake na
kwa kusimamia haki hasa pale zabuni zinapotangazwa. Aidha ametaka
mipango iliyowekwa kwenye mradi huo iheshimiwe ili thamani ya fedha
ionekane na wananchi wapate huduma kwa wakati.
Dkt. Biteko ameomba wananchi mkoani Kagera kuchangamkia fursa kutokana
na kuwepo kwa umeme wa uhakika mara baada ya miradi itakayofikisha
umeme mkoani humo kukamilika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatuma Mwassa amepongeza Serikali kwa
kuona umuhimu wa kutekekeza mradi huo wenye gharama kubwa ikiwa ni
kuonesha kwa vitendo jinsi inavyowajali wananchi hao.
Amesema wilaya zote mkoani Kagera zitaunganishwa na gridi kwani kwa
sasa no wilaya tatu tu ndio zimeunganishwa na Gridi ya Taifa.
Ameahidi kuwa, Wananchi katika mkoa huo watakuwa watumiaji wazuri wa
umeme na walipaji bili wazuri iili TANESCO iendelee kupata mapato ya
kutekeleza miradi mingine l.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa minne ambayo haijaunganishwa
kwenye gridi ya Taifa ikiwemo Rukwa, Lindi na Mtwara.
Amesema tukio la leo ni la kihistoria kwani kukamilika kusainiwa kwa
mikataba hiyo kunafanya mikoa yote iliyo nje ya gridi kuwa kwenye
mpango wa kupelekewa umeme gridi hivyo kwa sasa hakuna mkoa ulio nje
ya gridi ambao hauna mradi wa kupelekewa umeme.
Amesema kwa sasa Mkoa wa Kagera unapata umeme wa megawati 40 kutoka
nchini Uganda kupitia kituo cha Kyaka na megawati 7 kutoka mwekezaji
binafsi wa mradi wa Mirongo/ Kikagati.
Amesema wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani jumla ya
mikoa sita kati ya 26 haikuwa imeunganishwa kwenye gridi ya Taifa ila
kwa kipindi cha minne Serikali imefanikiwa kuunganisha umeme Kigoma na
Katavi huku mingine iiliyosalia ikiwa miaradi inayoendelea
kutekekelezwa.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO ),
Lazaro Twange mradi huo una umuhimu mkubwa mkoani Kagera kwani wilaya
za Kyerwa, Karagwe, Misenyi, Muleba, Bukoba Vijijini na Manispaa ya
Bukoba kwa muda mrefu sasa zimekuwa zikiitumia umeme kutoka nchini
Uganda takribani megawati 40 kupitia kituo cha kupoza umeme cha Kyaka
ambacho kinapokea umeme kutoka Masaka, Uganda kupitia njia ya umeme ya
msongo wa kilovoti 132 kufuatia mkataba wa makubaliano baina ya
Tanzania na Uganda.
Pia, kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kuunganishwa kwa kituo cha
kuzalisha umeme cha Kakono katika Gridi ya Taifa.
Amesema gharama za mradi ni shilingi bilioni 262.5 na utatekelezwa kwa
muda wa miezi 24.
Amesema Mradi huo unatekelezwa kwa fedha za Serikali kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo Mfuko wa Maendeleo wa Shirika
la Wauzaji Mafuta Duniani (OPEC) utachangia dola za Marekani milioni
60, Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi utachangia dola za Marekani
milioni 30, Mfuko wa Maendeleo wa Saudia utachangia dola za Marekani
milioni 13 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itachangia
dola za Marekani milioni 2.6 kwa ajili ya fidia kwa wananchi
watakaopisha mradi.
Amesema Wakandarasi watakaotekeleza mradi huo ni kampuni ya M/s. TBEA
Co. Ltd kutoka nchini China ambayo itahusika na ujenzi wa kituo cha
kupoza umeme cha Benako, na Kampuni ya M/s. Transrail Lighting Limited
kutoka India itahusika na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka
Benako hadi Kyaka.

No comments:
Post a Comment