Mwanahabari mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika vituo vya televisheni vya ITV na Azam TV, Allen Silvery Msungu, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani katika Kata ya Uleling’ombe, Jimbo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Msungu amekabidhiwa fomu hiyo leo, Agosti 19, 2025, mjini Morogoro na Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kamisheni na Uratibu wa CHAUMMA, David Chiduo.
No comments:
Post a Comment