BASHUNGWA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KARAGWE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 25, 2025

BASHUNGWA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KARAGWE.


Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe, Ndugu Alloys Simba Maira, amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Karagwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Innocent Bashungwa, leo tarehe 25 Agosti 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jimbo la Karagwe mkoani Kagera.

Makabidhiano hayo ni sehemu ya ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo Tume imetenga muda kuanzia tarehe 14 Agosti hadi 27 Agosti 2025 kwa wagombea wa nafasi ya Ubunge kuchukua fomu za uteuzi, hatua hiyo ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.


No comments:

Post a Comment