BASHUNGWA APONGEZA MENEJIMENTI YA IAA KWA MAFUNZO WALIYOTOA KWA WAFUNGWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 8, 2025

BASHUNGWA APONGEZA MENEJIMENTI YA IAA KWA MAFUNZO WALIYOTOA KWA WAFUNGWA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Innocent Bashungwa amempongeza Mkuu wa Chuo-IAA, pamoja na menejimenti nzima kwa namna anavyosimamia chuo, umahiri na ubunifu wake katika sekta mbalimbali ikiwemo mashirikiano aliyoanzisha na Jeshi la Magereza katika kutoa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wafungwa.

“Kama Mkuu wa Chuo pamoja na timu yako naomba tuwapongeze na tuwashukuru kwa ushirikiano, ambao mnalipa Jeshi la Magereza Katika hii programu ambayo leo hii tunatunuku wahitimu 170” amesema

Waziri Bashungwa ameyasema hayo Agosti 6, 2025 katika hafla ya kutunuku vyeti vya ujasiriamali na stadi za biashara kwa wafungwa waliohitimu mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara yaliyotolewa na Chuo Cha Uhasibu Arusha-IAA kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Arusha

Aidha, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Jeremiah Katungu amesema ana imani kubwa kuwa wahitimu wa mafunzo hayo wamepata elimu na maarifa muhimu, yatakayowawezesha kuwa wabunifu na wajasiriamali mahiri pindi watakapomaliza vifungo vyao na kwenda kwenye jamii.

“lengo la mafunzo ni kuwaandaa na kuwarejesha kwenye jamii wakiwa raia wema na wenye uwezo wa kuendesha shughuli za kiuchumi” amesema

Naye, Mkuu wa Chuo-IAA Prof. Eliaman Sedoyeka amemshukuru CGP Katungu kwa mashirikiano mazuri na IAA katika urekebishaji wafungwa, kupitia utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za biashara na kutoa rai kwa taasisi zingine za elimu, mashirika ya kiraia na taasisi binafsi kushirikiana na IAA katika kuhakikisha wafungwa wanapata ujuzi na maarifa.

Nao, baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyoanza Mei 7, 2025 wamepongeza  viongozi wote na walimu kutoka IAA kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali na stadi za biashara, wakisema italeta tija kwao kiuchumi baada ya kumaliza vifungo vyao.

No comments:

Post a Comment