BI. OMOLO APONGEZA WIZARA YA FEDHA NA TAASISI ZAKE KWA UTOAJI WA ELIMU MAONESHO YA NANENANE DODOMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 8, 2025

BI. OMOLO APONGEZA WIZARA YA FEDHA NA TAASISI ZAKE KWA UTOAJI WA ELIMU MAONESHO YA NANENANE DODOMA.

Naibu Katibu Mkuu (Huduma za Hazina), Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akipokea zawadi ya mfuko wenye machapisho mbalimbali kutoka kwa Afisa Mikopo wa Taasisi ya Self, Bi. Singoh Boniphace, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Afisa Habari Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Eva Valerian, akimweleza Kamishna Idara Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, majukumu yanayotekelezwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, akisikiliza elimu inayotolewa na Mkutubi Mwandamizi kutoka Kitengo cha Maktaba, Bw. Fredy Mpoma, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Kaimu Kamishna kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Bw. Bashiru Taratibu, akisoma kipeperushi cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025. Kushoto ni Afisa wa Kitengo hicho Bw. Fredrick Sanga.
Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Kilindimo, akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kuhusu mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya Serikali, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na taratibu za mikopo, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025. Kulia ni Mchumi Mwandamizi Wizara ya Fedha, Bw. Erick Mang’era.
Naibu Katibu Mkuu (Huduma za Hazina), Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watumishi kutoka Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma.) 


Na. Chedaiwe Msuya na Saidina Msangi, WF, Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, ametembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma ili kujionea huduma zinazotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake.

Bi. Omolo ameipongeza Wizara na Taasisi kwa kushiriki katika Maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “ChaguaViongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi2025’’, ili kufikisha elimu kwa wananchi hasa katika sekta ya kilimo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

‘‘Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuelimisha wananchi katika Maonesho haya hakika elimu mnayoitoa italeta tija katika utekelezaji wa majukumu ya wananchi ya kila siku hivyo kuchangia katika ukuaji wa sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na uchumi kwa ujumla’’, alisema Bi. Omolo.

Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake imetoa elimu kwa wananchi kuhusu Bajeti ya Serikali, Sera, uwekezaji, pensheni na mirathi, ununuzi wa umma na ugavi, masomo ya vyuo vya elimu ya juu, mifumo ya fedha, takwimu, rufaa za kodi, usuluhishi pamoja na huduma za kibenki.

No comments:

Post a Comment