CCM YAFUNGUA ZOEZI LA UREJESHAJI FOMU ZA URAIS INEC - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 27, 2025

CCM YAFUNGUA ZOEZI LA UREJESHAJI FOMU ZA URAIS INEC



Utaratibu wa urejeshaji wa fomu za wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais umeanza leo, Agosti 27, 2025, katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Njedengwa jijini Dodoma, ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa cha kwanza kufungua zoezi hilo.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mhe. Samia Suluhu Hassan, aliwasili katika Ofisi za INEC saa 1:52 asubuhi akiwa na mgombea mwenza wake, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele, alimtangaza rasmi Mhe. Samia Suluhu Hassan kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CCM.

No comments:

Post a Comment