KATIBU MKUU KIONGOZI ATOA MAELEKEZO, UZINDUZI SHIMIWI WAFANA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 2, 2025

KATIBU MKUU KIONGOZI ATOA MAELEKEZO, UZINDUZI SHIMIWI WAFANA



Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Wakati Katibu Mkuu Kiongozi akitoa maelekezo mahususi kwa washiriki na waandaaji wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), bonanza la uzinduzi wake lililofanyika kwa kuanza na mbio fupi fupi kwenye viwanja vya Bunge hadi uwanja wa Jamhuri limefana kwa kuudhuriwa na klabu mbalimbali.

Bw. Mululi Mahendeka, ambaye ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Ikulu, akimwakilisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka ameuelekeza uongozi wa SHIMIWI kuhakikisha inamuwasilishie orodha ya klabu zitakazoshiriki kwenye michezo hiyo itakayofanyika Jijini Mwanza kuanzia tarehe 1-16 Septemba 2025.

Bw. Mahendeka amesema utendaji kazi unajali matokeo hivyo ni lazima watumishi wanatakiwa kuwa na uadilifu, kujitolea, uzalendo na kujituma ni muhimu kwa kuwa ndio nguzo muhimu kwa kuhakikisha huduma bora kwa wananchi na kuimarisha ustawi wa jamii; pia amesisitiza watumishi kuongeza bidii makazini ili kufikia malengo yaliyowekwa nchini.

“Watumishi wahakikishe wanashiriki ipasavyo kwenye zoezi la uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, namtumie fursa hiyo ya kikatiba kuchagua viongozi na kuhamasisha wengine kwenda kupiga kura kwa utulivu na amani, nasisitiza pia mtekeleze wajibu wenu kwa kutoa huduma bora na kwa usawa kwa kipindi chote cha uchaguzi, na kushiriki kikamilifu maandalizi ya uchaguzi,” amesisitiza Bw. Mahendeka.

Halikadhalika, amewataka watumishi hao kuendelea kusimamia maadili mazuri ya utumishi wa umma kwa kujiepusha na vitendo vya rushwa michezoni na vitendo vingine vyovyote ambavyo vinakwenda kinyume na maadili ya umma.

Amesisitiza SHIMIWI na washiriki wote kwenda kutekeleza kaulimbiu ya michezo ya mwaka huu ya “Michezo kwa Watumishi huongeza tija kazini mjitokeze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu, kazi Iendelee”.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli amesema ofisi yake imepewa dhamana ya kusimamia watumishi wa umma na inatambua mchango wao kwa kiasi kikubwa katika kutoa huduma kwa wananchi.

“Uongozi wetu na Mhe Rias, na Katibu Mkuu Kiongozi na wote wanaohimiza ambao wanahimiza michezo mahala pa kazi, na kwa kwa niaba ya SHIMIWI tupo pamoja kuhimiza afya nzuri mahala pa kazi; na hususan watumishi waliopo Mji wa Serikali Mtumba wananafasi kubwa ya kufanya mazoezi kutokana na mazingira kuwa rafiki,” amesema Bi. Felister.

Ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuhakikisha wanafanya mazoezi kadri ya uwezo na nafasi zao kwa siku zote za juma.

Awali Mwenyekiti wa SHIMIWI, Bw. Daniel Mwalusamba amesema watumishi wa umma wanatoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa busara kwa kuendelea kuruhusu watumishi kushiriki michezo mahala pa kazi.

Bw. Mwalusamba amesema michezo hiyo itashirikisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, riadha, karata, bao, draft, mbio za baiskeli na darts.

Bw. Mjawa Sheduli aliyemwakilisha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala pa kazi (OSHA), amesema jukumu lao kubwa ni kulinda afya za wafanyakazi kuanzia akili na mwili, kwa kutoa ushauri ili wafanyakazi wasipate magonjwa mbalimbali.

Amesema wanaendelea kushirikiana na serikali, ili kulinda nguvukazi, iweze kuendelea kutekeleza majukumu yake, ambapo ameahidi kwa taasisi yake kuendelea kudhamini Bonanza la SHIMIWI, ikiwa sasa ni mwaka wa tatu.

No comments:

Post a Comment