
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara maarufu jijini Arusha,Ndugu Nathan Kimaro ametoa kiasi cha shilingi milioni 20 kama sehemu ya mchango wake wa kusaidia kampeni za uchaguzi wa wagombea wa Urais wa chama hicho Oktoba,2025.
Kimaro mbali ya kuchangia lakini pia alikuwepo ukumbini hapo jana Agosti 12,2025, kushuhudia ‘LIVE’ hafla hiyo ya Harambee ikiendelea ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Harambee hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Chama Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,ikilenga kukusanya kiasi cha fedha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Aidha katika harambee hiyo,Chama cha Mapinduzi (CCM) kilifanikiwa kuchangisha kiasi cha fedha, jumla ya shilingi Bilioni 86.31 zikiwemo na ahadi,ambapo kuchangia huko kutafika tamati Agosti 27,2025 .
No comments:
Post a Comment