NAIBU WAZIRI SANGU AONGOZA KURA ZA MAONI JIMBO LA KWELA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 5, 2025

NAIBU WAZIRI SANGU AONGOZA KURA ZA MAONI JIMBO LA KWELA



Na. Mwandishi Wetu- Sumbawanga


Aliyekuwa Mbunge wa Kwela mkoani Rukwa, Mhe.Deus Sangu ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ameongoza kura za maoni jimboni humo na kuwaacha mbali wapinzani wake wanne katika mchakato huo.

Matokeo yaliyotangazwa mapema leo Jumanne Agosti 6, 2025 Mhe.Sangu amepata kura 9,957, dhidi ya Justin Hiari aliyepata kura 2,973, Derick Sikale kapata 507, Walter Simsokwe kapata 112 na Yuster Bahati kaambulia kura 102


Taarifa za matokeo hayo zinaeleza kuwa jumla ya Wajumbe 13,496 walipiga kura ambapo kura halali zilikuwa 13,278 na kura 218 ziliharibika.

No comments:

Post a Comment