
NA MWANMDISHI WETU, MKURANGA
KUELEKEA Mitihani ya Taifa ya mwisho wa mwaka kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchini, Benki ya NMB imewataka wazazi na walezi kujikita katika ujenzi wa msingi imara wa kesho iliyo bora kwa watoto wao, kwa kuwazoesha utamaduni chanya kuweka akiba kwa ustawi na maendeleo ya kielimu na kimaisha.
Wito huo umetolewa na Meneja wa NMB Tawi la Mkuranga, Godwin Manimo, wakati wa Mahafali ya tatu na ya tano ya wanafunzi wa Kidato cha Nne na Darasa la Saba wa Shule za Sekondari na Msingi za Al-Rahmah, zilizo Mkuranga mkoani Pwani, zikiwa chini ya Kituo cha Maendeleo cha Al-Rahmah Development Complex.
Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba inayoandaliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itafanyika Septemba 10 na 11 mwaka huu, huku ile ya Kidato cha Nne ikitarajiwa kuanza Novemba 10, 2025, ambako wanafunzi wa Al-Rahmah wataungana na wenzao kote nchini, kuhitimisha hatua moja kielimu, kabla ya kuanza nyingine 2026.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo, yaliyodhaminiwa na NMB kupitia Akaunti za Mtoto na Chipukizi, Manimo aliwapongeza wazazi na walezi kwa upendo wa dhati, uwekezaji mkubwa kielimu na uwajibikaji wao kwa watoto katika kutimiza malengo ya vijana wao, walio kwenye mikono salama ya shule za Al-Rahmah.
“NMB tumedhamini mahafali haya kama ishara ya kuunga mkono juhudi za Al-Rahmah Complex, kuunga mkono uongozi wa shule hizi, ambao unafanya kazi kubwa, lakini pia kusapoti jitihada za walimu, ambao wanatoa maarifa chanya kwa watoto hawa, halikadhalika kwa wafanyakazi wengine wa Al-Rahmah ambao si walimu.
“Pamoja na kuunga mkono, kutambua na kuthamini kazi zenu, tumekuja hapa na masuluhisho maalum kwa watoto wetu, tumewaletea bidhaa mbili rafiki kwa vijana hawa, ambazo ni ‘NMB Mtoto Account’ na NMB Chipukizi Account,’ ambazo ni hatua muhimu katika kuanza safari ya malengo na kuwajengea watoto utamaduni chanya wa kuweka akiba.
“Hizi ni akaunti bora kabisa katika kuweka mipango ya akiba kwa watoto wetu, kila mzazi hapa anapaswa kutambua siri hii, kwamba wakati unatimiza malengo ya mwanao kielimu mwaka huu, utakuwa unahitaji fedha.








No comments:
Post a Comment