Na Mwandishi Wetu
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa umma kushiriki kwenye michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi.
Mhe. Rais ametoa kauli hiyo leo tarehe 14 Agosti, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa kwenye hafla ya kutunukiwa Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Kimatiafa (The Grand Cordon-CISM)
Amesisitiza kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ishirikiane na wizara zote nchini kuhimiza mazoezi sambamba na programu za kukuza vipaji.
“Hapa kuna yale mashindano yanayoshirikisha watumishi wa umma sijui yanaitwajwe SHIMIWI eeeeh na mawizara hawashiriki, sasa nikutake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo uwatake mawizara na mashirika kushiriki mashindano yale,” amesisitiza Mhe. Rais.
Pia amesisitiza kutaka taifa letu kuwa na uwakilishi thabiti kwenye mashindano mbalimbali Kimataifa na kuwa balozi wa amani.
Michezo ya SHIMIWI mwaka huu 2025 inatarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 1 hadi 16, Septemba, kwa kushirikisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, mbio za baiskeli, riadha, karata, bao, draft na darts.
No comments:
Post a Comment