WAANDAAJI WA BAJETI WATAKIWA KUZINGATIA VIPAUMBELE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 27, 2025

WAANDAAJI WA BAJETI WATAKIWA KUZINGATIA VIPAUMBELE


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiwataka Wataalam wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali kuzingatia vipaumbele vya miradi, wakati akifungua Kikao Kazi kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiteta jambo na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, wakati wa Kikao kazi cha Wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS), kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, akiwataka Wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, kuzingatia mafunzo kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS), yanayoendelea katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji wa Utendaji na Tathimini Tume ya Taifa ya Mipango Bi. Salome Kingdom, wakati wa Kikao kazi cha Wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS), kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wa kikao cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, kufanya Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2024/25 na Maandalizi ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2025/26, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika kikao hicho, jijini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wa kikao cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, kufanya Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2024/25 na Maandalizi ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2025/26, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika kikao hicho, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (katikati), Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji wa Utendaji na Tathimini Tume ya Taifa ya Mipango, Bi. Salome Kingdom wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wasaidizi wa Idara ya Bajeti pamoja na watoa mada katika Kikao kazi cha Wataalam wa uandaaji na usimamizi wa Bajeti ya Serikali kinachofanyika, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (katikati), Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji wa Utendaji na Tathimini Tume ya Taifa ya Mipango, Bi. Salome Kingdom wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya uandaaji wa Kikao kazi cha Wataalam wa uandaaji na usimamizi wa Bajeti ya Serikali kinachofanyika, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Josephine Majura na Peter Haule, WF, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amewataka Wataalam wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa miradi ili kuepuka kutekeleza miradi nje ya bajeti iliyopangwa.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma wakati akifungua rasmi Kikao kazi cha Wataalam wanaoandaa na kusimamia Bajeti ya Serikali awamu ya pili kuhusu kutumia Mfumo ulioboreshwa wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) katika kusimamia bajeti na kushauri namna bora ya kutekeleza bajeti zao.

Bw. Mwandumbya alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo wanaomba fedha za kutekeleza miradi nje ya bajeti mwezi mmoja baada ya bajeti kupitishwa jambo ambalo linatia mashaka katika upangaji wa vipaumbele vya utekelezaji wa bajeti.

Katika hatua nyingine aliwataka wataalamu hao kuangalia uwezekano wa kutekeleza miradi inayofanana kwa kushirikiana ili kuepuka kutumia rasilimali nyingi katika eneo moja ili kuleta tija.

“Yawezekana Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi zikawa na mradi wa umwagiliaji ambao utakidhi mahitaji ya mifugo na umwagiliaji lakini utakuta kila mmoja ana mradi wake, hili tunaliona ni changamoto kwa kuwa rasilimali ni zilezile, badala ya kuunganisha kuwa na mradi mmoja hata kama rasilimali itaongezeka kidogo kutakuwa na tija kuliko kila mmoja kutekeleza mradi wake”, alieleza Bw. Mwandumbya.

Aidha, alisema kuwa mwaka 2026/2027 utakuwa mwaka wenye bajeti inayotokana na vikaokazi vinavyoendeleza na utakuwa mwaka wa kwanza katika utekelezaji Dira ya Taifa ya 2050, hivyo ni vema kuangalia Dira inasemaje ili kuweza kupanga vizuri Bajeti kulingana na Dira hiyo.

Alisema kuwa katika kupanga bajeti ni lazima kuzingatia Dira ya Taifa lakini pia Ilani ya Chama ili kuwa na miradi ambayo inazingatia uelekeo wa nchi katika kipindi cha muda mfupi, wakati na mrefu ili kurahisisha upimaji.

Kikao kazi cha wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa kinatarajia kumalizika Agosti 29, 2025 kikijadili pia kuhusu mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/25, uandaaji wa bajeti ya 2025/26 na kupata maoni ya maandalizi ya Mwongozo wa uandaaji wa Mpango na Bajeti ya Serikali wa mwaka 2026/27.

No comments:

Post a Comment