
Dawati la Jinsia na Watoto Makao Makuu ya Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), limekabidhi pikipiki kwa maofisa wa dawati hilo kutoka mkoa wa Dodoma ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi, hasa katika kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.
Makabidhiano hayo yamefanyika Septemba 8, 2025 katika ofisi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ambapo pikipiki hizo zimeelekezwa kutumiwa katika wilaya za Dodoma Mjini, Chamwino, Mpwapwa, Kondoa, Chemba na Bahi kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa matukio, utoaji wa elimu kwa jamii na kurahisisha utoaji wa huduma kwa waathirika.
Akikabidhi pikipiki hizo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Pili Mande, Mratibu wa Kitengo cha Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net), amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuongeza ufanisi wa kazi kwa maofisa hao katika maeneo yao ya kazi.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha jamii inapokea huduma kwa haraka na kwa wakati, pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa kushirikiana na wananchi.










No comments:
Post a Comment