DODOMA YAPIGA HATUA KUDHIBITI UNYANG’ANYI NA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 2, 2025

DODOMA YAPIGA HATUA KUDHIBITI UNYANG’ANYI NA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI


Mkuu wa kitengo cha kampuni binafsi za ulinzi na Polisi Wasaidizi kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ulrich Matei, akiambatana na Katibu wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF NET), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pili Mande, wamefanya ziara ya kikazi mkoani Dodoma kwa lengo la kuimarisha utendaji wa Polisi Kata katika kuhudumia jamii.

Akizungumza na Wakaguzi Kata, DCP Matei amewataka kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu kwa kuzingatia kauli mbiu ya Jeshi la Polisi: *Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu*. Amepongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulinzi na usalama, ambazo zimechangia kudhibiti vitendo vya uhalifu, hasa unyang’anyi, kujichukulia sheria mkononi na wizi.

Kwa upande wake, SACP Pili Mande amesema Polisi Kata ni nguzo muhimu katika kusaidia jamii kujiepusha na uhalifu, huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (ACP) Galus Hyera akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya polisi na wananchi kupitia mikakati ya ulinzi shirikishi na ushiriki kwenye shughuli za maendeleo.

Ziara hiyo imelenga kuhimiza utekelezaji wa mwongozo wa mafunzo kwa Polisi Kata/Shehia ili kuboresha huduma kwa jamii.












No comments:

Post a Comment