Timu zatoa burudani murua katika SHIMIWI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 2, 2025

Timu zatoa burudani murua katika SHIMIWI



Na Mwandishi Wetu, Mwanza


Timu za michezo ya mpira wa netiboli, miguu na kuvutana kwa kamba kwa wanawake na wanaume, zimeendelea kutoa burudani safi kwa watazamaji wa michuano ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa mikoa (SHIMIWI) inayofanyika jijini Mwanza kwenye viwanja mbalimbali.

Matokeo ya michezo ya netiboli kwa asubuhi kwa timu zilizocheza kwenye uwanja wa CCM Kirumba ni Wizaraya Ujenzi imezidi kutakata kwa kushinda mechi mbili mfululizo baada ya leo kuwafunga ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa magoli 30-9; huku Wizara ya Elimu waliwafundisha Wizara ya Maji kwa magoli 21-16; nayo RAS Mara waliwaliza ndugu zao wa RAS Njombe kwa 28-8.

Katika michezo mingine timu ya Wizara ya Uchukuzi waliwafunga Wizara ya Mambo ya Ndani kwa 40-6; huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliwashinda RAS Iringa kwa 30-19; nayo OSHA waliwaliza TSC kwa 22-17; wakati Ukaguzi waliwachapa RAS Katavi kwa 55-8 na Mahakama waliwatia korokoroni GST kwa magoli 41-11.

Katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba timu ya Wizara ya Ujenzi walifuata nyao za dada zao kwa kuwashinda RAS Dodoma kwa magoli 3-2; huku timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliibuka kidedea mbele ya Waziri Mkuu Kazi kwa magoli 2-0 na TAKUKURU waliwashinda RAS Mwanza kwa 1-0; wakati katika mechi za uwanja wa Seminari ya Nsumba Katiba na Sheria waliwashinda Bunge kwa bao 1-0; huku RAS Simiyu wamefungwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mabao 2-0; na RAS Mara waliwabamiza Ukaguzi kwa mabao 2-1.

Michezo mingine iliyochezwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Bwiru timu ya Umwagiliaji waliwafunga RAS Kilimanjaro kwa 4-0; huku Uwekezaji walitoka sare dhidi ya RAS Manyara kwa 1-1 na Wizara ya Uchukuzi walitoka suluhu na Makamu wa Rais.

Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba iliyofanyika kwenye uwanja wa Furahisha kwa wanaume matokeo yakiwa kwenye mabano ni timu ya Uwekezaji waliwavuta RAS Pwani (1-0); Wizara ya Maliasili na Utalii wamewashinda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa (2-0); Katiba na Sheria waliwaliza Wakili Mkuu (1-0); nao Mashtaka waliwavuta Wizara ya Mawasiliano kwa (1-0) na Hazina waliwashinda RAS Geita kwa (2-0).

Michezo mingine Wizara ya Mambo ya Ndani waliwavuta RAS Iringa kwa (2-0); huku Wizara ya Uchukuzi wakiwasambaratisha Bunge kwa (1-0); nao Waziri Mkuu Sera waliwashinda Tume ya Sheria kwa (2-0); wakati Wizara ya Ardhi waliwafunga Maadili kwa (2-0); huku Mifugo waliwashinda UCSAF kwa (2-0); Wizara ya Maji walipata ushindi dhidi ya Wizara ya Viwanda na Biashara (1-0); Ofisi ya Rais Ikulu waliwashinda TAKUKURU (1-0) na Mahakama walipata ushindi wa chee baada ya Wizara ya Kilimo kutoonekana uwanjani.

Katika michezo ya wanawake timu ya Wakili Mkuu waliwashinda Wizara ya Viwanda na Biashara (1-0); Waziri Mkuu Sera waliwavuta ndugu zao Waziri Mkuu Kazi (2-0); Wizara ya Mambo ya Ndani waliwavuta Wizara ya Mawasiliano (2-0); Wizara ya Mifugo na Uvuvi walishinda Makamu wa Rais (1-0); timu ya Uwekezaji waliwashinda RAS Pwani (2-0) na Bunge walirudisha furaha kwa kuwavuta UCSAF (2-0).

Katika michezo mingine TAMISEMI waliwashinda RAS Shinyanga (2-0); huku Ofisi ya Taifa ya Mashtaka waliwavuta RAS Kilimanjaro (2-0); Wizara ya Madini waliwashinda Tume ya Utumishi (1-0); nao Haki waliwashinda Wizara ya Ardhi (1-0); Mahakama waliwavuta Katiba na Sheria (2-0); nazo timu zilizotoka suluhu ni TAKUKURU na RAS Tanga (0-0) na RAS Kagera dhidi ya Hazina.





No comments:

Post a Comment