NAIBU WAZIRI KIHENZILE AIPONGEZA TARURA UBORESHAJI WA BARABARA ZA WILAYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 15, 2025

NAIBU WAZIRI KIHENZILE AIPONGEZA TARURA UBORESHAJI WA BARABARA ZA WILAYA




Na Mwandishi Wetu, Arusha


Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kuleta mchango mkubwa kwenye sekta ya uchukuzi katika kuboresha miundombinu ya barabara za wilaya nchini ambazo zimewezesha kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea banda la maonesho la TARURA wakati akifungua Mkutano wa 18 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi unaofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

"Nawapongeza TARURA mnafanya kazi nzuri, mmekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha barabara za vijijini na mijini, hata bungeni wabunge tukisikia bajeti ya TARURA inaongezeka tunafurahia kwasababu tunajua huduma za usafiri na usafirishaji zinakwenda kuboreka ambapo wananchi wanapata nafuu kusafirisha mazao yao sokoni na kuzifikia huduma za kijamii kwa urahisi", amesema.

No comments:

Post a Comment