NAIBU WAZIRI KWAGILWA YUKO SALAMA BAADA YA KUPATA AJALI TUNDURU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 20, 2025

NAIBU WAZIRI KWAGILWA YUKO SALAMA BAADA YA KUPATA AJALI TUNDURU



Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Elimu, Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, yupo vizuri kiafya na timamu kuendelea na kazi baada ya tukio la ajali ya gari lililotokea majira ya saa tisa usiku wa Desemba 18, 2025 wilayani Tunduru, mkoa Ruvuma, akiwa safarini kuelekea mkoani Lindi.

Ajali hiyo ilitokea wakati Mhe. Kwagilwa akielekea mkoani Lindi kuungana na Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Mbeya, ambako pia aliambatana na Waziri Mkuu.

Gari lililopata ajali lilikuwa limewabeba watu wanne, akiwemo Mhe. Kwagilwa, Msaidizi wake Wakili Frank Nkya, Afisa Habari pamoja na Dereva.

Kwa mujibu wa taarifa za kitabibu, Mhe. Kwagilwa pamoja na wasaidizi wake wote waliokuwapo kwenye gari hilo wako salama kiafya.


Aidha mara baada ya kukamilisha taratibu za uchunguzi wa afya zao, Mhe. Kwagilwa na wasaidizi wake waliendelea na safari na tayari wameshaungana na msafara wa Mhe. Waziri Mkuu mkoani Lindi kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa majukumu ya kikazi.

No comments:

Post a Comment