
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeshiriki mkutano wa 18 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi unaofanyika Kwa siku tatu katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
TARURA inashiriki mkutano huo ikiwa ni mdau muhimu anayetoa mchango mkubwa kwenye sekta ya uchukuzi katika kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji.
Katika mkutano huo, Kaimu Meneja wa Usalama wa Barabara TARURA, Mhandisi Faizer Mbange ametoa wasilisho la utekelezaji wa shughuli za Wakala kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
TARURA pia inashiriki maonesho kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kauli mbiu ya mkutano huo kwa Mwaka huu ni "Mifumo Jumuishi ya Usafirishaji ni Msingi Muhimu wa Ukuaji wa Uchumi Kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Tanzania 2025".

No comments:
Post a Comment