VITUO VYA MAENDELEO YA VIJANA KUBORESHWA : NANAUKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 15, 2025

VITUO VYA MAENDELEO YA VIJANA KUBORESHWA : NANAUKA



Na: OR – MV, Songwe


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ameeleza dhamira ya Serikali katika kuboresha vituo vya maendeleo ya vijana nchini ili viwe chachu ya kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kielimu.

Hayo yameelezwa leo 15 Disemba, 2025 na Waziri Nanauka alipotembelea kituo cha Vijana cha Sasanda kilichopo mkoani Songwe kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa kituo hicho.

Waziri Nanauka amesema vituo hivyo vya Vijana vipo vitatu (3), kituo cha Sasanda – Songwe, Ilonga kilichopo Morogoro na Marangu kilichopo Kilimanjaro ambapo amesema vituo hivyo vina manufaa makubwa kwa vijana katika kuwajengea ujuzi wa vitendo, hivyo amesisitiza viongozi wa mikoa ambapo vipo vituo hivyo kuvipatia kipaumbele kwa kuwa ni sehemu zenye mazingira bora na fursa sahihi kwa vijana waliopo katika maeneo hayo kushiriki katika Maendeleo ya Taifa kupitia shughuli watakazofanya kituoni humo.

“Kituo hiki cha Sasanda kilianza kutoa mafunzo kwa vijana toka mwaka 1979 na mara ya mwisho kituo hicho kutoa mafunzo ilikuwa mwaka 2008, hivyo kwa muda mrefu kimekuwa hakifanyi kazi, hivyo tumejipanga kuboresha vituo hivi na kuona tunawezaje kuwasaidia vijana waliopo katika haya maeneo” amesema

Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya Maendeleo ya vijana nchini na kuamua kuunda wizara maalumu inayoshughulika masuala yao.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapana amewakumbusha Watendaji wa Serikali kuendana na falsafa za Wizara hiyo ambazo ni kuwa na kasi kwenye masuala ya vijana, kutembeelea maeneo ambayo vijana wanapatikana na amehamasisha matumizi ya teknolojia kwenye kufanikisha masuala ya vijana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja wa wananchi wanaoishi karibu na Kituo hicho Bw. Eliano Mwashiozya wamefurahishwa kuona ujio wa Waziri wa Maendeleo ya Vijana na wameshukuru serikali kwa mpango wa kuboresha kituo hicho cha maendeleo ya vijana na ameseema kitasaidia kupunguza changamoto za ukosefu wa ajira, kuongeza kipato cha vijana sambamba na kuwajengea uwezo vijana wa kushiriki katika shughuli za uzalishaji.


No comments:

Post a Comment