WASTAAFU DODOMA MJINI WANAOLIPWA NA HAZINA WAANZA KUPEWA VITAMBULISHO VYA KIELEKTRONIKI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, December 16, 2025

WASTAAFU DODOMA MJINI WANAOLIPWA NA HAZINA WAANZA KUPEWA VITAMBULISHO VYA KIELEKTRONIKI.


Mhasibu Mkuu Daraja la kwanza kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Jenipha Ntangeki, akizungumza kuhusu zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielekroniki kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina, katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo, linalofanyika katika Ofisi za Hizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mhasibu Mkuu Daraja la kwanza kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Jenipha Ntangeki, akionesha moja ya kitambulisho cha kielektroniki ambavyo vimeanza kugawiwa kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina, katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo, linalofanyika katika Ofisi za Hizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mhasibu Mwandamizi Pensheni, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Mwakabango, akimkabidhi kitambulisho cha kielektroniki Mstaafu Hezron Bitesigirwe, katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo, linalofanyika katika Ofisi za Hizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mtunza Kumbukumbu Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Farida Mlanda, akimkabidhi kitambulisho cha kielektroniki mstaafu Andrew Makulukulu, katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo, linalofanyika katika ofisi za Hizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mhasibu Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mfaume Uledi, akimsaidia mstaafu Wilbroad Makarabo, kuhakiki taarifa zake kabla ya kukabidhiwa kitambulisho kipya cha kielektroniki, katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo, linalofanyika katika Ofisi za Hizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mtunza Kumbukumbu Wizara ya Fedha, Bi. Gladness Malisa, akimkabidhi kitambulisho cha kielektroniki mstaafu Willbroad Makarabo, katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo, linalofanyika katika Ofisi za Hizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.


Wizara ya Fedha imetoa wito kwa Wastaafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini wanaolipwa na Hazina kufika katika Ofisi za Hazina Dodoma ili kupatiwa vitambulisho vya wastaafu vya kielektroniki.

Wito huo umetolewa na Mhasibu Mkuu Daraja la kwanza kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Jenipha Ntangeki, katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, wakati wa zoezi la kutoa vitambulisho vya kielektoniki kwa wastaafu kutoka Wilaya ya Dodoma Mjini ambalo limeanza rasmi kufanyika Mjini Dodoma na linatarajiwa kuendelea kwa muda wa siku kumi na nne.

‘‘Vitambulisho hivi ni tofauti na vya zamani ambavyo vilikuwa katika karatasi ambayo pia utunzaji wake ulikuwa changamoto ndio maana tumekuja na vitambulisho vya kielektroniki ambavyo ni imara na pia vitawawezesha Wastaafu wetu kupata huduma bila changamoto kwa kuwa taarifa zao zitasomeka kwa urahisi kielekroniki,’’ alisema Bi. Ntangeki.

Alisema vitambulisho hivyo vinafaa kwa matumizi rasmi hivyo wastaafu waliokabidhiwa vitambulisho vyao wanaweza kuanza kuvitumia kupata huduma bila changamoto kutokana na kuwa vitambulisho hivyo ni vya kisasa na imara.

Akizungumza kwa niaba ya Wastaafu waliofika Ofisi za Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata vitambulisho vipya Bw. Andrew Makulukulu, aliishukuru na kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha, kwa kuendelea kuwajali kwa kuwapatia vitambulisho hivyo ambavyo vitawaondolea changamoto ya taarifa zao kutokusomeka.

‘’Serikali imefanya jambo la maana sana kuja na vitambulisho hivi, nawakumbusha wastaafu wenzangu ambao wanalipwa pensheni na Hazina waje hapa viwanja vya Treasury Square kuchukua vitambulisho vyao’’ alisema Bw. Makulukulu.

Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la kugawa vitambulisho kwa wastaafu na kwa sasa limeanza katika Wilaya ya Dodoma Mjini na linatarajia kuendelea kutolewakwa wastaafu wengine wanaolipwa mafao yao na Hazina katika mikoa mingine nchini mapema Januari Mwakani 2026 kwa ratiba itakayotangazwa kupitia vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment