WIZARA YA FEDHA YAITA WADAU KUTOA MAONI YA KUBORESHA MWONGOZO WA USIMAMIZI WA MALI ZA SERIKALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 17, 2025

WIZARA YA FEDHA YAITA WADAU KUTOA MAONI YA KUBORESHA MWONGOZO WA USIMAMIZI WA MALI ZA SERIKALI


Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Baadhi ya wadau wa kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia mjadala wa utoaji maoni, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Ismael Ogaga, akizungumza na wadau katika kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ajali na Fidia, Wizara ya Fedha, Dkt. Wenceslaus Sobayi, akizungumza na wadau katika kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Msimamizi wa Mali za Serikali Mwandamizi Wizara ya Fedha Bw. Michael Luziga, akiwasilisha Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kwa wadau wa kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya hiyo kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Afisa Ugavi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Revocatus Tesha, akitoa maoni kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, katika kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ajali na Fidia, Dkt. Wenceslaus Sobayi, na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo ya Usimamizi wa Mali za Serikali Ismael Ogaga, wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kikao kazi cha kukusanya maoni kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.



Matukio mbalimbali katika kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichowakutanisha Wasimamizi wa Mali wa Mikoa (M), Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Watumishi wa Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Saidina Msangi na Silya Kombe, WF, Dodoma.


Wizara ya Fedha imetoa rai kwa wadau kutoa maoni yatakayowezesha kuboresha Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025 utakaosaidia kusimamia mali zilizo kwenye Taasisi za Umma kwa tija na ufanisi zaidi ili kuimarisha na kuboresha huduma zinazotolewa na Serikali kupitia mali hizo.

Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, wakati akifungua kikao kazi cha kukusanya maoni ya wadau kutoka taasisi 25 za Umma zinazowakilisha Mkoa wa Dodoma, Wasimamizi wa Mali wa Mikoa kutoka mikoa saba (7), Wasimamizi wa Mali za Serikali kutoka Ofisi ya Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma, kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Bw. Sendo alisema, Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2025, ambao wadau wanatarajiwa kutoa maoni ya kuuboresha inatokana na fursa mbalimbali zilizojitokeza katika usimamizi wa mali za umma katika kipindi cha utekelezaji wa Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma wa mwaka 2019.

‘‘Nawaasa kila mmoja wetu ahakikishe anashiriki kikamilifu kwa kutambua kuwa Mwongozo huu ni nyenzo muhimu itakayowezesha usimamizi bora wa Mali za Umma katika Taifa letu ikizingatiwa kuwa kwenye Rasimu hii ya Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma, masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa mali yameelezwa ikiwemo majukumu na wajibu wa usimamizi wa Mali za Umma kwa Watendaji, Wakuu wa vitengo na Wakuu wa Idara mbalimbali katika Taasisi za Umma,’’alisema Bw. Sendo.

Aliongeza kuwa rasimu hiyo pia imejumuisha usimamizi wa mali chini ya ushirikiano wa umma na binafsi (PPP-Projects), Upatikanaji wa mali, matumizi ya mali, usimamizi wa mali za miradi, kushughulikia ajali na potevu za mali za Umma, Ufutaji na uondoshaji wa mali chakavu pamoja usajili wa vyombo vya moto.

Alisema kuwa mwongozo huo utakapokamilika na kusainiwa na Mlipaji Mkuu wa Serikali (PMG) utaanza kutumika pamoja na Kanuni za Usimamizi wa Mali za Umma za mwaka 2024 hivyo kuwataka kujadili kwa uwazi ili kujenga uelewa wa pamoja katika suala la usimamizi wa mali za umma na kuhakikisha utendaji bora ,uwajibikaji wa kifedha na utoaji wa huduma bora.

Bw. Sendo aliwasisitiza wadau hao kuhakikisha kuwa Mwongozo huo utakapokamilika unatumika kikamilifu ili kutumia fursa zilizopo na zitakazojitokeza baadaye katika usimamizi wa mali za umma.

Aidha, Bw. Sendo alieleza kuwa Wizara ya Fedha imepewa jukumu la usimamizi wa Mali za Umma kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma, Sura 348 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2024 ambapo hutekeleza jukumu hilo kupitia Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali (GAMD) yenye ofisi zake za mikoa ambazo zinahudumia taasisi zote za Umma zilizopo katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.

‘‘Kutokana na wingi wa rasilimali mali tulizonazo inatupa picha ya wingi wa gharama ambazo Serikali imekuwa ikizitumia katika upatikanaji na utunzaji wa mali hizo, hii inatupa kila sababu ya kuwa na mikakati madhubuti ya kuzisimamia mali hizo ili ziweze kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na kuiwezesha Serikali kupata manufaa ya uwekezaji uliokusudiwa kwa kipindi kirefu’’, alifafanua Bw. Sendo.

Aliongeza kuwa Wizara ya Fedha ikiwa na dhamana ya Usimamizi wa Mali za Umma nchini imefanya jitihada mbalimbali katika kuongeza ufanisi wa Usimamizi wa Mali za Umma nchini ikiwemo kusimika na kuwezesha matumizi ya mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mali za Serikali “Government Assets Management Information Systems - (GAMIS) ambao unatumika kutunza na kuchakata taarifa za mali za Taasisi zote za Umma nchini.

Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho Msimamizi wa Mali za Serikali Mkoa wa Tabora, Bi. Karerema Kwareh, alieleza kuwa kikao hicho kitawawezesha wadau kujadiliana kwa kina kuhusu mwongozo huo na kujenga uelewa wa pamoja utakaowezesha kuwa na mwongozo sahihi katika usimamizi wa mali za umma.

Kikao kazi hicho cha siku moja kiliandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Mali za Umma kimekutanisha wadau kutoka taasisi 25 za Umma zinazowakilisha Mkoa wa Dodoma, pamoja na Wasimamizi wa Mali wa Mikoa kutoka mikoa saba (7), sambamba na Wasimamizi wa Mali kutoka Ofisi ya Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment