MHE. MUNDE AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MADINI YA GRAPHITE MOROGORO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 23, 2026

MHE. MUNDE AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MADINI YA GRAPHITE MOROGORO


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) akisisitiza kuongeza kasi ya kuanza kwa Mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite uliopo Mahenge Mkoa wa Morogoro, wakati wa mkutano na Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited uliongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) akipokea zawadi ya Kofia kutoka kwa Kiongozi wa Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ambaye ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, baada ya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa mradi wa huo, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) akiagana na Meneja Mkuu wa Uhandisi na Masuala ya Kiufundi wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited, Bw. Daniel Pantany, baada ya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite mkoani Morogoro, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kiongozi wa Ujumbe Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, akieleza manufaa ya Mradi wa madini ya Graphite wakati wa mkutano na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhandisi na Masuala ya Kiufundi Kampuni hiyo, Bw. Daniel Pantany.

Ujumbe wa Wizara ya Fedha ukiwa katika mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Ujumbe Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, kuhusu utekelezaji wa mradi wa Madini ya Graphite ulioko mkoani Morogoro, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma

Ujumbe Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, ukiwa katika mkutano na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), kuhusu utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite ulioko mkoani Morogoro, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) akiongoza mkutano kati yake na Ujumbe Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, kuhusu utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite mkoani Morogoro, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa nne kulia) na Kiongozi wa Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa pande hizo mbili, baada ya mkutano utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite Morogoro, uliofanyika Ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)


Na. Peter Haule na Jordan Mbwambo, WF, Dodoma


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amehimiza utekelezaji wa Mradi wa uchimbaji madini ya Graphite uliopo Mahenge Mkoa wa Morogoro ili uanze kutoa manufaa yaliyotarajiwa kwa watanzania kwa wakati.

Rai hiyo imetolewa Ofisini kwake jijini Dodoma wakati wa mkutano kati yake na Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims.

Mhandisi Munde alisema kuwa, Serikali itaendelea kutoa msaada katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo unaokwenda sambamba na wajibu wa mwekezaji katika masuala ya uwazi, utii wa masharti yaliyowekwa na ushirikiano wa karibu na mamlaka husika kadri utekelezaji unavyoendelea.

“Napenda kuihimiza kampuni yenu kuhakikisha kuwa mchakato wa upatikanaji wa mtaji unakamilika ndani ya muda uliokubaliwa ili kuanza utekelezaji wa mradi na kwamba fedha hizo zinaelekezwa kwa mujibu wa taratibu zilizokubaliwa”, alisema Mhandisi Munde

Alisema kuwa Serikali inatarajia mchango wa mradi huo katika upatikanaji wa ajira, kukuza fursa za biashara za ndani, kuongeza mapato ya fedha za kigeni, kuendeleza mnyororo wa thamani wa madini ya Graphite, kukuza viwanda, pamoja na kuongeza mapato ya muda mrefu ya Serikali yanayotokana na ushiriki wake katika mradi huo.

Vile vile alieleza kuwa mradi huo utatoa kipaumbele kwa maudhui ya ndani (local content), ikiwemo matumizi ya bidhaa na huduma za ndani, na pale ambapo ushiriki wa nje utahitajika, kutakuwa na utaratibu unaohakikisha ushiriki wa wazawa usiopungua asilimia 30, kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo.

Aidha, Mhandisi Munde aliihakikishia Kampuni hiyo kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono uwekezaji wa kimkakati unaoendana na vipaumbele vya maendeleo ya Taifa ikizingatiwa kuwa mradi huo ni sehemu ya nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika madini muhimu duniani.

Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ambaye ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims, alisema kuwa mradi utasaidia katika maendeleo ya viwanda na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika usambazaji wa madini muhimu yanayotumika katika uzalishaji wa kisasa na teknolojia za nishati safi.

Bw. Sims ameahidi kuongeza jitihada katika kuhakikisha mtaji unapatikana kwa haraka na kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na aliomba Serikali kuendeleza ushirikiano na wadau muhimu ili kufanikisha mradi huo kuanza kwa wakati.

No comments:

Post a Comment