OMR YAFUZU KWA KISHINDO 16 BORA MEI MOSI, 2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 20, 2026

OMR YAFUZU KWA KISHINDO 16 BORA MEI MOSI, 2026

Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ‘Netiboli’ ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifanya mazoezi ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo baina yao na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi yanayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026
Benchi la Ufundi la Timu ya Mpira wa Pete ‘Netiboli’ ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia mchezo baina ya Timu hiyo na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.
Kocha wa Timu ya Mpira wa Pete ‘Netiboli’ ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mafuru Buriro akifuatilia mchezo baina ya Timu hiyo na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika harakati za kugombea mpira na Wachezaji wa Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais akifunga goli wakati wa mchezo baina ya timu hiyo na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.

Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuelekea Uwanjani kuumana na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.
Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuelekea Uwanjani kuumana na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.
Benchi la Ufundi la Timu ya Mpira wa Pete ‘Netiboli’ ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia mchezo baina ya Timu hiyo na Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Michezo ya Mei Mosi inayoendelea katika Uwanja wa Mji Mwema, Mkoani Njombe Aprili 19, 2026.

Timu ya Mpira wa Pete ‘Netiboli’ ya Ofisi ya Makamu wa Rais imefanikiwa kutinga kwa kishindo hatua ya 16 bora ya Michezo ya Mei Mosi, 2026 kwa kuifunga Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mabao 52 kwa Tano (05).

Katika mchezo huo uliofanyika jana jioni (Aprili 19, 2026) katika Uwanja wa Mji Mwema, uliopo Halmashauri ya Mji Njombe, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kuifanya Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kushindwa kutoa ushindani uliotarajiwa.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mafuru Buriro amesema ushindi huo umeonesha dhamira ya kikosi hicho kutaka kuonesha ushindani katika mashindano hayo ili kufika hatua za juu.

“Tayari tumetambua ukubwa na ubora wa timu tulizokabiliana katika hatua ya makundi. Dhamira yetu baada ya kufika hatua ya 16 bora ni kuongeza juhudi, uwezo na maarifa ili kufika mbali zaidi” amesema Buriro.

Akizungumzia mchezo wa hatua ya 16 bora, Buriro amesema kikosi hicho kimepanga kuendeleza wimbi la ushindi na hali hiyo inachochewa na ushindi wa michezo mitatu ya Timu hiyo katika hatua ya makundi ambapo imeweza kukusanya alama sita na kuongoza kundi H lililokuwa na Timu nne.

Ameeleza kuwa pamoja na kushiriki kwa mara ya kwanza katika michezo ya Mei Mosi, wachezaji wa kikosi hicho wameonesha ukomavu wa hali ya juu na kukabiliana vyema na timu zenye upinzani mkali uwanjani.

Kwa upande wake, Katibu wa Michezo Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Marwa Nyaisawa amebainisha siri ya kikosi cha timu hiyo kufanya vizuri inatokana na hali ya umoja, upendo na mshikamano baina ya wachezaji na benchi la ufundi.

“Tumekuwa tukifanya vizuri katika mechi zetu kutokana na mshikamano uliopo ndani ya kambi sambamba na kujenga hali ya kujiamini kwa wachezaji wetu tangu tulipowasili hapa Njombe” amesema Nyaisawa.

Aidha Nyaisawa ametaja siri nyingine ni ushirikiano inaopatiwa Timu hiyo na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya kambi ya timu hiyo kwa kuwapa morali wachezaji na benchi la ufundi.

Kabla ya kutinga hatua ya 16 bora, Timu ya Netiboli ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilizifunga Timu za Wizara ya Maji (26-20), Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma (27-11) kabla ya kuitandika bila huruma Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (52-05).

Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora katika mchezo wa mpira wa pete ‘Netiboli’ ni Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Ofisi ya Rais IKULU, Wizara ya Maji, Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Timu nyingine ni Wizara ya Fedha, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mahakama ya Tanzania, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Michezo ya Mei Mosi, 2026 ni sehemu ya shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani inayoadhimishwa tarehe 1 Mei yakibeba kauli mbiu isemayo “Michezo kwa Afya, Ajira, Furaha na Kazi Inaendelea; Kazi zenye staha ni Nguzo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira 2050”.

No comments:

Post a Comment