OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAOMBA BUNGE KUIIDHINISHIA ZAIDI YA BILIONI 99 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 21, 2026

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAOMBA BUNGE KUIIDHINISHIA ZAIDI YA BILIONI 99


Na Okuly Julius, OKULY BLOG


Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) imeomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi zaidi ya bilioni 99 kwa ajili ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Muungano, mazingira na miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti bungeni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 23.29 zimetengwa kwa ajili ya Fungu 26 (Ofisi binafsi ya Makamu wa Rais). Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 1.29 ni mishahara huku shilingi bilioni 22 zikiwa ni matumizi mengineyo.

Aidha, Serikali imeomba kuidhinishiwa shilingi bilioni 76.69 kwa ajili ya Fungu 31, zitakazotumika katika matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 38.37 ni kwa matumizi ya kawaida, ambapo shilingi bilioni 4.88 ni mishahara ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, shilingi bilioni 7.10 ni ruzuku ya mishahara kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), na shilingi bilioni 26.40 ni matumizi mengineyo.

Kwa upande wa miradi ya maendeleo, jumla ya shilingi bilioni 38.31 zimetengwa, ambapo shilingi bilioni 14.40 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 23.91 ni fedha za nje.


Kwa ujumla, bajeti hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa Muungano, kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment