
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji limetupilia mbali shauri la Klabu ya Simba lililokuwa likipinga uhalali wa usajili wa mchezaji Mohamed Damaro Camara kuchezea Yanga SC.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 2, 2026, Simba iliwasilisha malalamiko ikidai kuwa usajili wa Camara unaifanya Yanga kuwa na wachezaji 13 wa kigeni badala ya 12, jambo ambalo walidai linakiuka Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu pamoja na kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Hata hivyo, Kamati hiyo imeamua kuwa usajili wa Camara uko sahihi na haukiuki kanuni zilizotajwa na Simba, hivyo kutupilia mbali hoja zote za mlalamikaji.
Uamuzi kamili wa shauri hilo unatarajiwa kuwasilishwa rasmi kwa klabu ya Simba kwa taratibu za kikanuni.

No comments:
Post a Comment